LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 5, 2021

JKT YAMWAGIWA NEEMA YA SOKO LA MAHINDI YA NJANO TANI MILIONI MOJA+video

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya (kushoto) na  Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge wakitiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika sekta ya ya kilimo ambapo pamoja na mambo mengine suala la kutafutiwa masoko limo.


 Mahindi ya njano



Na Richard Mwaikenda, Dodoma.


Wizara ya Kilimo, imelitafutia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), soko la mahindi ya njano tani milioni moja Misri.


Neema hiyo ya soko la mahindi ya njano, imetangazwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Gerald Kusaya katika hafla ya kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika sekta ya kilimo iliyofanyika hivi karibuni Makao Makuu ya jeshi hilo, wilayani Chamwino, Dodoma.


Amesema moja ya mambo watakayoshirikiana na JKT ni kuwatafutia masoko ya mazao kabla ya hata kuanza kuzalisha ili kuwa na uhakika ya kuyauza, hivyo ameihimiza JKT kaunza haraka kulima zao hilo ili kukidhi soko hilo.


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Kusaya akielezea kuhusu soko hilo...


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages