LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 21, 2021

MAGUFULI ALIKUWA NI RAIS WA PEKEE, MZALENDO NA ALIJITOA KWA AJILI YA TAIFA-ASKOFU CHANDE+video

Aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli.
ASKOFU Dk. Evance Chande wa Kanisa la EAGT Nazaret, Ipagala jijini Dodoma, akizungumza na vyombo vya habari kuhusu msiba mzito uliolikumba Taifa kuondokewa na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Magufuli.


Kanisa la EAGT Nazaret Ipagala, Dodoma


Na Richard Mwaikenda, Dodoma ASKOFU Dk. Evance Chande wa Kanisa la EAGT Nazaret, Ipagala jijini Dodoma, amesema Taifa limempoteza aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli ambaye alikuwa rais wa pekee, mzalendo na aliyejitoa kwa ajili ya Taifa letu. Maneno hayo ameyatoa alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kanisani kwake hivi karibuni ambapo amesema karne ya 21 tumepoteza mtu muhimu, rais wa mfano, kwani alipoingia madarakani hakuwa na tamaa ya kwenda kutembea nje ya nchi zaidi ya nchi chache za Afrika Mashariki. "Alikuwa na juhudi za kuhakikisha Tanzania inakuwa ya mabadiliko, aliamua kujitoa kwa hali yoyote kusaidia watanzania... ...Rais Hayati Magufuli alikuwa ni rais wa wanyonge, mama lishe, machinga walifanya shughuli zao bila kubughudhiwa, alisaidia masikini wasio na kitu, ndiyo maana hata akisafiri akiona mtu analia alikuwa anasimamisha msafara na kumuuliza unalia nini na kumsaidia," amesema Askofu Dk. Chande. Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video Askofu, Dk. Chande akizungumza mengi kuhusu msiba huu mkubwa uliolikumba Taifa letu... Imeandaliwa na Richard Mwaikenda Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 0754264203
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages