Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Magu,Zabron Makoye, aliagiza jana kuwa kwa vile kwenye mradi huo kuna nguvu za wananchi halmashauri ihakikishe inakamilisha darasa lililobaki kwa fedha za mapato ya ndani.
“Hii itatuletea shida na nguvu hizo za wananchi zitatuumiza maana unapovunja majengo unawakatisha tamaa, tafuteni fedha mkamilishe madarasa wakati uchunguzi ukifanyika na atakayebainika kuhusika alitafuna fedha awajibike,”aliagiza Makoye na kuongeza;
Alieleza kuwa madarasa hayo matatu yaliyojengwa kwa michango ya wananchi, yalivunjwa kwa maagizo ya Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu kwa madai kuwa yalijengwa chini ya kiwango.
Mary alieleza zaidi kuwa wananchi walianzisha ujenzi wa madarasa hayo matatu kwa nguvu zao,kabla ya Septemba 2020 kupokea fedha za EP4R sh.milioni 40 ambazo zimekamilisha madarasa mawili tu badala ya matatu.
Aliongeza kuwa mhandisi wa halmashauri, Mhandisi Msisdn Ok, kabla ya ujenzi wa madarasa hayo kuanza aliwashauri waweke nondo nne kila upande ili kuufanya msingi wake kuwa imara baada ya kukaa muda mrefu bila kujengwa lakini aligeuka na kuagiza yavunjwe.
“Cha kushangaza mhandisi huyo alifika na tape akidai hawezi kuchezea kazi yake kwani miradi mikubwa ya aina hiyo inaweza kumwingiza kwenye matatizo akaagiza madarasa yavunjwe ingawa Mwenyekiti wa Halmashauri wa wakati huo, Elisha Hilal, aliagiza ujenzi uendelee ili kutowavunja moyo wananchi,”alisema Mary.
Alisema binafsi aliumizwa sana kuvunjwa kwa madarasa hayo ambayo ndani yake kuna nguvu za wananchi,ili kutowaumiza watoto halmashauri ikae na kutafuta fedha ikamilishe jengo lililobaki wakati wakisubiri ukaguzi ufanyike wa matumizi ya fedha za EP4R.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Magu, Simon Mpandalume, alisema hawakuridhishwa na fedha hizo sh. milioni 40 kujenga madarasa mawili tu na hivyo waliagiza ufanyike ukaguzi maalum (Special Auditing)kujiridhisha zilitumikaje.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇