LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 10, 2021

MSAFARA WA MAKAMU WA PILI WA RAIS WAPATA AJALI ENEO LA KITOGANI, ZANZIBAR, MMOJA AFARIKI

Habari tulizopata hivi punde zimedai kuwa msafara wa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar umepata ajali katika eneo la Kitongani mjini Zanzibar na inaelezwa kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa na mmoja amefariki dunia.


Kwa mujibu wa habari hizo, gari lililokuwa limebeba Waandishi wa habri katika msafara huo limepinduka mara nne na kusababisha kifo na majeruhi kadhaa ambao idadi yo bado haijajulikana.


Inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni gari moja aina ya Escudo lenye rangi nyeupe lililokuwa likiendeshwa na mzungu mmoja ambalo baada ya kupita msafara wa polisi na Makamu wa Pili wa Rais lilichomoka na kutaka kuendelea na safari wakati msafara wote haujamalizika.


Kwa mujibu wa habari hizo baada ya hapo dereva wa gari lenye waandishi alihofia kugongana uso kwa uso na gari hilo la mzungu akaamua kwenda pembeni hatua iliyofanya gari kupinduka na kwamba baadhi ya  majeruhi ambao idadi yao haijatajwa wamepelekwa haraka Hospitali ya Makunduchi ambako wamelazwa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages