Naibu Waziri wa Kilimo mhe, Hussein Bashe Kushoto akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa wizara hiyo Bwana Gerald Kusaya Kulia.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji akitoa maelekezo kwa Wakala wa mbegu za kilimo ASA makaomakuu Morogoro kabla ya kukagua Maabara ya mbegu pamoja na ghala la kuhifadhia mbegu za kilimo.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji pamoja na wafanyakazi wa Wakala wa Mbegu za Kilimo ASA wakiwa katika Picha ya pamoja.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bwana Bakari Msulwa kushoto akiangalia mbegu za kilimo zinazozalishwa na Wakala wa mbegu ASA.
********************************
Na Farida Said, Morogoro.
Wakala wa Taifa wa mbegu za kilimo(ASA) wameshauriwa kujikita katika uzalishaji wa mbegu za zao la Alizeti ili kumaliza kabisa tatizo la uhaba wa mafuta ya kupikia ,ambayo kwa asilimia kubwa serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuagiza mafuta hayo kutoka njee ya nchi.
Wito huo umetolewa Mkuoani Morogoro na kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakati ilipotembelea Wakala huo na kasha kukagua Maabara ya mbegu za kilimo pamoja na Ghala la kuhifadhia mbegu, ambapo wameishauri taasisi hiyo kujikita katika uzalishaji wa Mbegu za Alizeti.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Dokta Christina Ishengoma amesema Serikali ione umuhimu wa kuiwezesha ASA kutimiza majukumu yake kwa lengo la kuzalisha mbegu za kutosha kwa ajili ya wakulima.
Kwa Upande wake Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda amesema Wizara inampango wa kumaliza tatizo la upungufu wa mbegu kwa kushirikiana na taasisi zake zilizoko chini ya Wizara ya kilimo ikiwemo TOSCI,ASA na TARI ili kuliwezesha Taifa kuwa na mafuta pamoja na chakula Cha uhakika.
“Serikali imejipanga kuhakikisha upatikanaji wa mbegu kupitia ASA baada ya kuboresha miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba yote yanayozalisha mbegu za kilimo”..alisema Dokta Mkenda.
Aidha Prof. Mkenda ameongeza kuwa Wizara itaongeza nguvu kwenye Taasisi ya Utafiti ya Kilimo Tanzania (TARI) ili kuwezesha utafiti wa mbegu Hali itakayosaidia wakulima kupata Mbegu zinye ubora na kuhakikisha mashamba yote ya ASA yanapata wekewa miundombinu ya umwagiliaji hatua inayolenga kuwezesha kupatikanaji wa Mbegu bora za kilimo na za uhakika.
Awali Mkurugenzi mkuu wa Wakala wa Taifa wa Mbegu za Kilimo (ASA) Dokta Sophia Kashenge, ameeleza changamoto mbalimbalia zinazoikabili taasisi hiyo ikiwemo mgogoro wa shamba la Msimba lililopo Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro pamoja na upungufu wa Maghala ya kuhifadhia Mbegu zinazozalisha na ASA.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇