Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Zainab Chaula akiwa na Wadau wa Jamii ya Dijitali baada kupiga nao picha alipofungua kikao cha wadau hao cha kujadili mkakati wa kukuza na kuendeleza matumizi ya TEHAMA katika vituo vya afya na shule za msingi na sekondari nchini kilichofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Zainab Chaula akizungumza alipokuwa akifungua kikao cha wadau cha kujadili mkakati wa kukuza na kuendeleza matumizi ya TEHAMA katika vituo vya afya na shule za msingi na sekondari nchini. Kikao hicho kilifanyika jijini Dodoma leo Februari 23,2021.
Baadhi ya wadau wa jamii ya Dijitali wakiwa katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Mifumo ya Habari na Rasilimali Watu wa Shirika la Misada la Marekani, Desderi Wengaa akizungumza wakati wa kikao hicho kuhusu umuhimu wa Tehama.
Katibu Mkuu, Dk. Chaula akiwa katika picha ya pamoja na wadau hao.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.. Zainab Chaula
amesema kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Sekta binafsi katika
kukuza na kuendeleza matumizi ya TEHAMA katika Sekta ya afya na elimu nchini.
Dkt
Chaula ameyazungumza hayo jijini Dodoma leo Februari 23,2021, alipokuwa akifungua kikao cha Wadau wa Jamii ya Kidijitali cha kujadili
mkakati wa kukuza na kuendeleza matumizi ya Tehama katika vituo vya afya na shule
nchini.
Mdau nakuomba uendelee kusikiliza Dk. Chaula na wadau wakizungumza kupitia clip hii ya video kuhusu namna ya kuboresha mifumo ya Tehama katika sekta hizo...
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇