LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 16, 2021

AMANI NA URAFIKI, NDIO UJUMBE MUHIMU ZAIDI WA MAZOEZI YA PAMOJA YA KIJESHI YA BAHARINI YA IRANI NA URUSIA

Amani na urafiki, ndio ujumbe muhimu zaidi wa mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya baharini ya Iran na Russia

Msemaji wa mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya baharini ya ukanda wa amani 2021 yanayoshirikisha majeshi ya Iran na Russia amesema, mazoezi hayo yanyaoanza leo yanafanyika kwa kufuata kalenda ya kila mwaka ya nchi washiriki; na ujumbe wake muhimu zaidi ni amani na urafiki.

Mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya baharini ya Iran na Russia 2021, yameanza leo asubuhi katika eneo la kaskazini ya Bahari ya Hindi na Bahari ya Oman na yataendelea kwa muda wa siku mbili hadi kesho.

Katika mkutano na waandishi wa habari aliofanya pamoja na kamanda wa msafara wa manowari za Russia, Admeri Gholamreza Tahani ameeleza kuhusu umuhimu wa eneo la kaskazini ya Bahari ya Hindi na kufafanua kuwa, kaskazini ya Bahari ya Hindi kuna malango bahari matatu kati ya matano ya kistratejia duniani, ambayo ni lango bahari la Hormuz lililoko kaskazini, lango bahari la Malacca lililoko mashariki na lango bahari la Bab-el-Mandeb lililoko magharibi ya eneo la kaskazini ya Bahari ya Hindi; na kwa kuzingatia safari za meli za kibiashara na meli za mafuta katika eneo hilo hasasi, udharura wa kuhakikisha usalama wa safari za kibiashara za baharini umeongezeka maradufu.

Manowari ya Iran

Admeri Tahani amesema: "eneo la kaskazini ya Bahari ya Hindi halikabiliwi na tishio lolote, na sisi tunafanya mazoezi katika eneo hilo lenye usalama ili kutoa mafunzo ya ustadi wa kiwango cha juu kabisa kwa askari wa vikosi vya majini kwa ajili ya maeneo yasiyo na usalama".

Msemaji wa mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya baharini ya ukanda wa amani 2021 yanayoshirikisha majeshi ya Iran na Russia amekumbusha pia kwamba, "kwa mwaka wa pili mfululizo, vikosi vya majini vya kistratejia vya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu na kikosi maalumu cha majini cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) vimekuwa wenyeji wa manowari za jeshi la Russia; na kwa kuzingatia mipango makini iliyopangwa na kuratibiwa katika muda wa mwaka mmoja uliopita, tunatumai kuwa operesheni zilizoratibiwa kwa ajili ya mazoezi hayo zitatekelezwa kwa ufanisi na kwa namna bora kabisa".../

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages