MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamepangwa Kundi A pamoja na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na El Marreikh ya Sudan katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yenye washambuliaji Watanzania, Thomas Ulimwengu na Eliud Ambokile imepangwa Kundi B na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Al Hilal ya Sudan na CR Belouizdad ya Algeria.
Wydad Casablanca yenye kiungo mshambuliaji Mtanzania, Simon Msuva imepangwa Kundi C na Horoya AC ya Guinea, Petro Atletico ya Angola na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Vigogo wa Tunisia, Esperance wao wamepangwa Kundi D na vigogo wa Misri, Zamalek, MC Algiers ya Algeria na Teungueth ya Senegal.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇