LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 4, 2021

MILIONI 3 SADAKA ZA UTOAJI MAJINI ZAMFANYA CHANDE AMILIKI KAMPUNI MBILI KUBWA DODOMA




Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Sahl Investment Co, Ltd, inayomiliki pia kampuni tanzu ya Sahl Real Estate na Sahl Printing akifungua mlango wa  moja ya magari yake mbele ya ofisi yake iliyopo Uzunguni,Kilimani, Dodoma. PICHA ZOTE NA NA RICHARD MWAIKENDA

                                Ismail Chande
Operater Maimuna Shaban akiuendesha mtambo wa kuchapisha mabango mbalimbali. 

Muonekano  kwa nje katika kiwanda chake cha uchapishaji cha Sahl Printing eneo la Uzunguni, Kilimani, Dodoma.



Na Richard Mwaikenda, Dodoma.

KILA mwenye mafanikio katika maisha yake iwe kibiashara, kielimu au kwa kupitia kilimo na mambo mengine, huwa na siri yake moyoni kuhusu mafanikio hayo.


Mfanyabiashara Ismail Chande ameamua kuweka hadharani siri ya mafanikio yake aliyoyapata ndani ya miaka minne ya utawala wa Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli.


Chande, mzaliwa wa Wilaya ya Liwale mkoani Lindi, ambaye kwa takribani miaka 20 ameishi na kusomea mkoani Arusha, anataja siri ya mfanikio yake kuwa ni sh mil. 3, alizokuwa anapewa sadaka na aliokuwa anawatoa majini.


Anasema kazi yake kubwa ambayo ameizoea ni utoaji watu majini ambayo imefikia yamemzoea na yeye ameyazoea kiasi cha kuwa kama ndugu.


 "kazi moja kubwa ambayo naifanya sana, mimi huwa nawasomea sana watu kuwatoa majini, hatimaye majini yamenizoea na mimi nimeyazoea, tunaelewana vizuri na imekuwa kama ndugu, hivyo pesa milioni tatu niliyoipata kama sadaka kutoka kwa watu hao niliifanya kuwa mtaji,"anaelezea kwa misitizo.


Anasema mwaka 2016 alihamia Dodoma na mwaka 2017 aliamua kutumia fedha hiyo kufungua kampuni ya Sahl Imvestment ambayo ndani yake ilianzishwa kampuni ya Real Estate na baadaye mwaka 2020 akafanikiwa kuanzisha kampuni nyingine ya uchapishaji mabango na bidhaa zingine iitwayo Sahl Printing.Chande ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hizo.


Kampuni ya Real Estate hadi sasa inamiliki viwanja vyenye hati 125 eneo la Mtumba, Chamwino karibu Ikulu viwanja 300, Nala karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma viwanja 120 pamoja na mashamba. Pia karibu na Hospitali ya Uhuru wanamiliki viwanja 11 vilivyopimwa na kupata kibali cha kujenga apartment 50.


Pia Chande anaelezea jinsi alivyofanikiwa kujenga Dodoma nyumba yake ya kuishi  na kununua gari pamoja na kuanzisha biashara zake zingine.

Aidha kutokana na mafanikio aliyoyapata kupitia  kmpuni zake hizo, Chande anasema ameamua kutoa shukrani kwa chama chake Chama Cha Mapinduzi kwa kuingia makualiano na Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa Dodoma, kujenga jengo la maduka kwa gharama ya sh. mil. 52 eneo la Uzunguni, Kilimani Dodoma amapo pia yeye ni mpangaji.


Kiwanda cha Sahl Printing  kilichopo eneo la Uzunguni kilimani,Dodoma,huchapisha kwa bei poa bidhaa zifuatazo;


LARGE FORMAT;

Roll up banners, Back Drop Banners, Tear Drop Banners, 3D Letters & Acrylic, Pylons, Billboards, Vinly Stickers, Car Branding na Sign Boards.


STATIONERY MATERIALS;

Broshure, Flyers, ID Cards, Company Profile, Posters, Book Covers & Publication  na Letter Heads.


 PROMOTIONAL MATERIALS;

Mug (Cup printing), Pen, Gazebo, Wheel Covers, Press Banner, Moile Cases, Badges, T-shirts printing.


Ndugu msomaji sina haja ya kuendelea kuelezea, bali nakuomba uendelee kumsikiliza Chande kupitia Clip hii ya video hapa chini akielezea ni jinsi gani amefanikiwa katika biashara zake kupitia mtaji huo.


 

IMEANDALIWA NA; RICHARD MWAIKENDA MHARIRI LOG YA TAIFA YA CCM 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages