Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetekeleza mara moja kazi ya kupeleka huduma kwa wakazi wa Mtaa wa Golani, Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam.
Kazi inayofanyika sasa ni ulazaji wa mabomba ya ukubwa wa inchi 12, 10 na 8 kwa umbali wa kimometer 6.1.
Mapema Desemba 24, 2020, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alitembelea eneo la Golani na kuagiza DAWASA kupeleka huduma ya maji mara moja ili wananchi wa eneo hilo waondokane na changamoto ya upatikanaji huduma ya Majisafi.
Kukamilika kwa mradi huu kutanufaisha wakazi takribani 5000.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇