LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 2, 2021

MBUNGE SICHALWE AIANGUKIA SERIKALI, AOMBA TARURA IONGEZEWE BAJETI MOMBA


  

MBUNGE wa Jimbo la Momba, Condester Sichalwe ameiomba Serikali kuiongezea bajeti Wakala wa Barabra Vijijini Tanzania (TARURA) ili iweze kumudu kuzihudumia takriani barabara 57 zilizomo jimboni humo.

Akiwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya barabara na kushiriki ujenzi, Sichalwe amesema licha ya jimbo hilo kuwa na mito mingi mikubwa na midogo, lakini inaponyesha mvua huchafua mito na kuharibu miundombinu ya barabara hali ambayo inawawia vigumu Tarura kuzifanyia matengenezo kutoka na ufinyu wa bajeti. 

Aidha, Sichalwe ameiomba Tanroads kuchukua jukumu la kuzihudumia baadhi ya barabara zinazounganisha wilaya na mikoa, ili kuipunguzia mzigo Tarura.

Ndugu wadau mnaofuatilia utendaji wa Mbunge huyu mwana mama jabali, Condester Sichalwe nawaomba niwaache msikilize anachokizungumza kupitia clip hii ya video... 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages