CHALINZE, Pwani
Wakazi wa Chalinze mkoa wa Pwani kwa sasa wanaweza kunufaika na huduma bora na haraka ya kupiga na kupokea simu, intaneti na huduma za kifedha kwa simu za mkononi baada ya Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel Tanzania kuzindua Mfumo bora na wa kisasa wa mtandao wa 4G pamoja na maduka mapya ya kisasa ya Airtel Money Branches wiliayani humo.
Maduka hayo mapya wilayani humo yatakuwa yanatoa huduma za salio au floati kwa mawakala wao wadogo, kuhudumia wateja muhimu pamoja na wateja wengine kwenye huduma za SIMSWAP, kusajili laini mpya kwa alama ya vidole, kurudisha laini iliyopotea pamoja na huduma zingine nyingi.
Akizunguma na wakazi wa Chalinze wakati akizindua moja kati ya maduka hayo mjini Chalinze, Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete aliishukuru Airtel Tanzania kwa uamuzi wake wa kufungua maduka mapya wiliyani humo kwani kwa sasa wananchi watakuwa na huduma ya mawasiliano kwa urahisi.
‘’Kama sote tunavyo fahamu ya kwamba mji wa Chalinze ni muhimu sana kwani unaunganisha miji mingine ya nchi yetu. Vile vile, tunazo vyanzo vyetu vya mapato ambazo vinachangia uchumi wetu na hivyo kufunguliwa kwa maduka haya ya Airtel Chalinze kutachangia sana ukuaji wa uchumi wetu.
Nawaomba wananchi wenzangu wajitokeze kupata huduma kwenye maduka haya kwani kuna huduma mbali mbali kama kubadilisha laini za simu zetu kwenda kwenye Mfumo wa 4G, kusajili laini mpya kwa alama ya vidole, kurudisha laini iliyopotea pamoja na huduma zingine nyingi,’ alisema Kikwete.
Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema kuwa kampuni ya Airtel imedhamiria kuja na huduma ambazo zinapatikana kwa unafuu, za kipekee na rahisi kutumia pamoja na bidhaa ambazo zinakidhi mahitaji ya wateja wa Airtel. Vile vile, tumekuwa tukifanya juhudi Kubwa kuhakikisha tunaleta huduma karibu na wateja wetu kwani ndio watu muhimu sana kwenye biashara yetu. Airtel imekuwa ikifungua maduka haya ili kufikisha huduma zake karibu na wananchi ambao ndio wateja wake.
Aliongeza, ‘kufungua kwa maduka haya hapa wilayani Chalinze ni mkakati wa kupanua huduma za rejareja ambao ni mpango endelevu wa kampuni ya Airtel kufikisha huduma bora kwa wateja wake. Moja ya lengo letu Kubwa ni kuwa suluhisho la kifedha hapa nchini.
Airtel inatoa huduma bora za suluhisho la kifedha hapa nchini kupitia Airtel Money na kwa vile mtandao wetu umeenea kote nchini, tunayo uhakika kuwa tutaendelea kuwa bora hata kwa jamii zetu zinazoishi maeneo ya vijijini kwani hata maduka yatakuwa yanapatikana maeneo hayo.
‘Airtel imejitolea kuboresha huduma za kifedha kwa kuwafikia zaidi ya Watanzania asilimia 80 ambao hawana huduma za kibenki hapa nchini. Airtel imekuwa ikibuni huduma ambazo ni za kipekee za Airtel Money ambazo ni nafuu na zinapatikana kwa urahisi kwa vile kutoa huduma za mikopo maarufu kama Timiza Loans, group loans – Timiza Vicoba pamoja na kuunganisha kwenye Mfumo wa malipo ya serikali ambapo wateja wanaweza kulipia malipo na bili mbali mbali’.
Airtel Money pia imeunganisha na benki zaidi ya 40 ambapo wateja wa Airtel Money wanaweza kutoa na kuweka pesa moja kwa moja kwa kupitia akaunti zake za Airtel Money.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇