LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 30, 2020

WANANCHI SHINYANGA WASHAURIWA KUTUMIA AIRTEL MONEY KWA AJILI YA USALAMA WA PESA ZAO

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Boniface Chambi akizindua Maduka hayo unaoenda sambamba na kuhamashisha wakazi wa mkoa wa Shinyanga kutumia huduma ya Airtel ya 4G yenye kadi na teknolojia ya kisasa ya mawasiliano. Katibu Tawala huyo alifuatana na Ofisa Mauzo was Airtel Mkoa wa Shinyanfa Ezekiel Emmanuel (kushoto) na mhudumu was duka Salma said (kulia).


Shinyanga, Disemba 30, 2020

Wakazi wa mkoa wa Shinyanga wameshauriwa kuwa na mazoea ya kutunza fedha zao kwenye akaunti ya Airtel Money ili kupunguza uwezekano wa kuibiwa au kupoteza pesa zao kwani Airtel Money ni huduma yenye usalama wa hali ya juu.


Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa mkoa huo Boniface Chambi wakati akizindua duka jipya na la kisasa mjini Shinyanga. 


"Nimepewa taarifa ya huduma na bidhaa nyingi zinazotolewa na kampuni ya Airtel na kwa kweli nimefurahi sana. 


Moja ya huduma ambayo ningependa kuwasisitiza wakazi wa Shinyanga kuwa na kawaida ya kuitumia kila wakati ni huduma ya Airtel Money’, alisema Chambi.


‘Huduma hii ni salama kwa kutuma fedha na pia kwa kupokea. Kuna wakazi wengi waliopo huko vijijini na san asana kwenye machimbo ya madini ambako hakuna huduma za kibenki. 


Nawashauri kuwa wawe na kawaida ya kutumia huduma ya Airtel Money kuepuka wizi wa fedha zao,’ aliongeza Chambi huku akisema Airtel inao mawakala kila sehemu kwa hivyo pia inakuwa ni rahisi kutoa fedha zao pale wanapohitaji kuzitumia.


Chambi aliipongeza kampuni ya Airtel kwa kuweza kupeleka huduma zake karibu na wateja kwani inaonyesha ni jinsi ngani kampuni hiyo imejiandaa kuwahudumia Watanzania bila kujali mahali waliopo.


‘Nawaomba wakazi wenzangu wa mkoa wa Shinyinga kuendelea kutumia huduma na bidhaa zinazotolewa na Airtel kwani ni kampuni yao. ‘Airtel inamilikiwa na Watanzania kwa asilimia 49 kupitia kwa Serikali ya Muungano wa Tanzania. Unapokuwa unatumia huduma na bidhaa za kampuni hii ya Airtel ni kwamba unatumia kile kilicho cha kwako’, Chambi alisema.


Kwa upande wake, Afisa mauzo wa Airtel Tanzania mkoani Shinyanga Ezekiel Emmanuel alisema kuwa Airtel mkoani Shinyanga imejipanga kuhakikisha kuwa Airtel inaleta karibu huduma zake kwa wananchi ili kufanya mawasiliano yawe nafuu.


‘Kwa hapa mkoani Shinyanga tunao maduka kama haya takribani 49. Kwa hapa mjini tunayo maduka matatu na hii yote ni kuhakikisha kila kona huduma na bidhaa za Airtel zinapatikana kwa urahisi,’ alisema Emmanuel huku akisema kuwa Airtel inao mawakala 657 ambao wanatoa huduma za Airtel Money mkoani kote Shinyanga.


Vile Vile, Airtel mkoa wa Shinyanga tunajivunia kuunga mkono juhudi za kutoa ajira kwa vijana wa Kitanzania. 


Mawakala hao 657 ni vijana tuliowapa mafunzo na kisha wakajiajiri wenyewe kutoa huduma za Airtel. Wanapata kipato cha kuendesha Maisha yao ya kila siku kwa kutoa huduma za Airtel, tunajivunia sana kwa hilo – alisema Emmanuel.


Uzinduzi wa maduka hayo unaenda sambamba na kuhamashisha wakazi wa mkoa wa Shinyanga kutumia huduma ya Airtel ya 4G yenye kazi na teknolojia ya kisasa ya mawasiliano.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages