Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mwalimu Josephat Maganga akihutubia na
kuipongeza Shule ya Ellen White kwa mafanikio makubwa iliyopata kwa muda mfupi wa miaka miwili tangu ianzishwe 2019.
Amesema mafanikio ya shule hiyo yanaipaisha kielimu wilaya
hiyo pamoja na mkoa wa Dodoma kwa rekodi hiyo ya kuwa ya shule ya kwanza kufaulisha kati ya
shule 14 zenye idadi ndogo ya wanafunzi 40 wilayani humo katika matokeo ya
darasa la saba mwaka huu.
Pia imekuwa shule ya pili kwa Mkoa wa Dodoma.
Kwa habari zaidi sikiliza kwenye video clips zilizopo chini.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Ellen White iliyopo Nzuguni jijini
Dodoma, Phien Maiko akielezea historia ya shule hiyo, changamoto na mafanikio
wakati wa mahafali ya kwanza ya
waliomaliza darasa la saba yaliyofanyia Desemba 6, 2020.
DC Maganga akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo, Samwel Ikwabe kwa mafanikio hayo.
Waalimu wa shule hiyo wakiimba wimbo kunogesha mahafali
DC ,Maganga akikata keki iliyoandaliwa maalumu kwa ajili ya mahafali hayo
DC Maganga akiwakabidhi vyeti na zawadi baadhi ya walimu na
watumishi wa shule hiyo kwa kutambua mchango wao kufanya shule hiyo kuwa kinara.
DC Maganga akiwakabidhi vyeti wanafunzi waliomaliza darasa
la saba shuleni hapo.
Mkurugenzi Mtendaji, Samwel Ikwabe akitoa shukrani viongozi na wageni waalikwa walihudhuria mahafali hayo. Kulia ni Sospeter Magina mthibiti ubora wa elimu.
Wanfunzi wa shule hiyo wakiimba wimbo wa kuwaaga waliomaliza darasa la saba
Mmoja wa wazazi wa watoto wanaosoma shuleni hapo akielezea kufurahishwa na mafanikio ya ya shule hiyo na kwamba wasije wakabweteka bali wayaendeleze.
Wanafunzi waliomaliza darasa la saba shuleni hapo
wakitumbuiza kwa wimbo.
Baadhi ya wazazi na wageni waalikwa
Wanafunzi wa shule ya awali katika shule hiyo wakitumbuiza kwa wimbo wakati wa mahafali hayo. |
MWALIMU MKUU PHIEN MAIKO AKIELEZEA HISTORIA YA SHULE HIYO, CHANGAMOTO PAMOJA NA MAFANIKIO
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇