Na Richard Mwaikenda, Dodoma
ZAIDI ya viongozi waandamizi 20 wa mataifa mbalimbali duniani wamethibitisha kuhudhuria hafla ya kuapishwa Rais Mteule Dk. John Magufuli kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Kati ya viongozi hao yupo, Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, Rais wa Zimbabwe, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Nabii TB Joshua wa Nigeria.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Hassan Abbas alipozungumza na vyombo vya habari kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya kuapishwa kwa Dk Magufuli kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Abbas amesema kuwa sherehe hizo pia zitahudhuriwa na zaidi ya mabalozi 83 wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Pia sherehe hizo zitanogeshwa na wasanii maarufu nchini wakiwemo akina, Diamond, Ali Kiba, Hamonize, Zuchu, Nandy na wengine wengi.
Milango ya kuingilia uwanjani hapo itafungulia mapema saa 12 asubuhi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇