LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 10, 2020

NDUGAI ATWAA TENA USPIKA, AAHIDI KULIFANYA BUNGE LA KIPEKEE TANGU UHURU


IMG_20201110_112418_465
Spika wa Bunge Job Ndugai akiongoza kikao baada ya kuaoishwa.


Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limemchagua mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, kuwa Spika wa Bunge la 12, baada ya kupata ushindi wa kura kwa asilimia 99.7.


Katika uchaguzi uliofanyika hii leo Novemba 10, 2020, Bungeni Dodoma, Ndugai amepigiwa kura na wabunge wateule 344 kati ya wabunge 345 na kura ya hapana ilikuwa ni moja.


 Awali akiomba kura kwa wabunge hao, Ndugai amesema kuwa Bunge la 12 litakuwa ni Bunge bora na lenye mfano wa kuigwa kuliko mabunge yoyote yale na kwamba katika Bunge hilo hakutakuwa na kambi rasmi ya upinzani Bungeni kwa kuwa hawajatimiza asilimia 12.5, kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages