LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 9, 2020

MBUNGE MTEULE WA KONGWA AONGOZA USAJILI WA WABUNGE, APOKEA BEGI KUTOKA BENKI YA CRDB

Mbunge Mteule wa Kongwa, Job Ndugai akifanyiwa usajili na Afisa wa Bunge, Monica Mwamnyange ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya Bunge la 12 linalotegemewa kuanza tarehe 10 Novemba, 2020 tukio lililofanyika leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Mbunge Mteule wa Kongwa, Job Ndugai (wa pili kulia) akikabidhiwa begi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kushoto) tukio lililofanyika leo katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto). Benki ya CRDB imetoa Mabegi 400 kwa Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mbunge Mteule wa kongwa, Job Ndugai akizungumza na ugeni kutoka CRDB Benki ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela (kulia kwake), Maafisa Waandamizi kutoka Ofisi ya Bunge na Waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa mabegi 400 kwa Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tukio lililofanyika leo katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai

 Mbunge Mteule wa Kongwa, Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Waheshimiwa Wabunge wakati wa usajili unaoendelea leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya Bunge la 12 linalotegemewa kuanza tarehe 10 Novemba, 2020 Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages