LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 9, 2020

RAIS DK. MAGUFULI AMUAPISHA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Adelardus Lubango Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika hafla iliyofanyika katika viwanja wa Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 09 Novemba 2020. 
Rais Dk. John Magufuli na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakiwa katika Picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa serikali Profesa Adelardus Lubango wakati wa hafla hiyo.

FULL STORY👇

Rais Dk. John Magufuli leo amemuapisha Prof. Adelardus Lubango Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika hafla ambayo imefanyika Ikulu, Chamwino jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge Job Yustino Ndugai, Jaji Mkuu Ibrahim Hamis Juma, Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na viongozi wengine mbalimbali.

Akizungumza baada ya kumuapisha Mhe. Rais Magufuli amesema Watanzania wana matumaini makubwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wanataka kuona Serikali yao inapata uwakilishi mzuri katika masuala ya kisheria, hivyo amemtaka kuhakikisha anasimamia vizuri kesi za Serikali na kuzitetea kwa uharaka mali za Serikali.

“Watanzania hawapendi kuona Serikali yao inashindwa katika kesi, kachape kazi, kawatetee Watanzania hasa wanyonge, katetee mali za Serikali na kwa haraka. Umefanya kazi nzuri katika kipindi chako cha kwanza, nataka ukafanye kazi vizuri zaidi, ukajipange sawasawa, ndio maana nakupongeza lakini wakati huo huo nakupa pole kwa majukumu haya” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amewatoa hofu viongozi wateule wote ambao wamekuwa na hofu ya kuondolewa ama kubadilishwa katika nafasi walizonazo baada ya yeye kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili, akisema hatarajii kufanya mabadiliko ya viongozi hao labda kwa wale watakaokuwa wanastaafu ama kutofanya vizuri katika majukumu yao.

“Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi, Viongozi wa Taasisi na Idara za Serikali na wengine wote chapeni kazi, simuondoi mtu kwenye nafasi yake labda aharibu yeye mwenyewe au astaafu” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages