Waziri Mkuu mstaafu John Samweli Malecela akiagana na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama. Alihudumu kipindi cha Rais Ali Hassan Mwinyi.
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye akiagana na viongozi wa Ulinzi na Usalama baada ya kuhudhuria sherehe hizo. Alihudumu kwa kipindi cha miaka 10 wakati wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin Mkapa.
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akienda kupanda gari baada ya kuhudhuria sherehe hizo muhimu. Alihudumu miaka mitatu wakati wa Rais wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete.
Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda akiagana na viongozi wa Ulinzi na Usalama baada ya kuhudhuria sherehe hizo. Alihudumu miaka 7 wakati wa Rais wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete.
Waziri Mkuu aliyestaafu mara baada ya Rais Magufuli kuapishwa, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama mara baada ya sherehe hizo kumalizika.
Mwingine aliyehudhuria lakini hatukubahatika kupata picha yake ni Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba ambaye alihudumu wakati wa Rais wa Awamu ya Kwanza, Hayati Julius Nyerere na kipindi kifupi cha Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.
Wengine waliowahi kutumikia nafasi ya Uwaziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini wametangulia mbele ya haki ni; Hayati Rashid Mfaume Kawawa, Edward Moringe Sokoine na Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika mara baada ya kupata Uhuru 1961.
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri wa CCM Blog.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇