LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 6, 2020

MARAIS WASTAAFU MWINYI, KIKWETE WALIVYOHUDHURIA KUAPISHWA KWA DK MAGUFULI

Rais mstaafu wa Awamu ya Pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi akiagana na wakuu wa vyombo vya Uinzi na Usalama baada ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Dk. John Magufuli kuwa Rais wa Tanzania kipindi cha pili mjini Dodoma Novemba 5, 2020. Mwinyi aliongoza mwaka 1985-1995. Pia aliwahi kuwa Rais wa Zanzibar 1984- 1985. PICHA ZOTE NA RICHARD MAIKENDA
Mwinyi akiondoka baada ya kuhudhuria sherehe hizo.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete akizungumza na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo alipokuwa akiondoka baada ya kushiriki kwenye sherehe za kuapishwa kwa mara ya pili Dk. John Magufuli kuwa Rai s wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kikwete aliongoza Tanzania  kwa miaka kumi kuanzia mwaka 2005 hadi 2015. 
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Generali Mabeyo.

 Kikwete akiaga wananchi uwanjani baada ya kuhudhuria sherehe hizo.
Rais mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya 6, Aman Abeid Karume akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Mabeyo.
Rais mstaafu wa Awamu ya 7 wa Zanzibar,  Dk. Ali Mohamed Shein akiondoka uwanjani baada ya kuhudhuria sherehe hizo. Shein ambaye amemkabidhi madaraka Rais wa Awamu ya Nane wa Zanzibar, Dk. Mwinyi, pia alikuwa Makamu wa Rais wakati wa Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin Mkapa na miaka mitano ya kwanza ya Rais wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete.
Makamu wa Rais mstaafu, Dk.  Mohamed Bilal akiwa na wake zake wawili, akijiandaa kuondoka uwanjani baada ya kuhudhuria shere hizo. Dk. Bilal alitumikia nafasi hiyo miaka mitano ya Rais wa Awamu ya Nne, Dk.Kikwete.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages