TANGAZO LA KUITA WABUNGE DODOMA KUHUDHURIA MKUTANO WA KWANZA WA BUNGE LA KUMI NA MBILI
Kufuatia Tangazo la Rais la kuitisha Bunge
lililotangazwa kwenye Gazeti la Serikali, Toleo Maalum (Special Supplement) la tarehe 5 Novemba, 2020 (Tangazo Namba 942A) na kufuatia Tangazo
nililolitoa kwenye Gazeti la Serikali Toleo Maalum (Special
Supplement) la tarehe 5 Novemba, 2020 (Tangazo Namba 1763A) kuhusu nafasi ya Spika kuwa wazi na utaratibu
utakaotumika kujaza nafasi hiyo, pamoja na Gazeti la Serikali, Toleo Maalum (Special
Supplement) (Tangazo Namba 1764A) kuhusu nafasi ya Naibu Spika kuwa wazi na
utaratibu utakaotumika kujaza nafasi hiyo na Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi
hao, Wabunge wote wanafahamishwa kwamba shughuli za usajili na taratibu
nyingine za kiutawala zitafanyika Ofisi ya Bunge Dodoma kuanzia tarehe 7 – 9
Novemba, 2020.
Hivyo basi, Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kwanza
wa Bunge Jipya kitafanyika tarehe 10 Novemba, 2020 kama ilivyotamkwa kwenye
Tangazo la Rais. katika Mkutano huu wa kwanza wa Bunge la 12, shughuli
zitakazofanyika ni pamoja na:
(a)
Kusomwa Tangazo la Rais la kuitisha Bunge
(b)
Uchaguzi wa Spika
(c)
Kiapo cha uaminifu kwa Wabunge wote
(d)
Kuthibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu
(e)
Uchaguzi wa Naibu Spika
(f) Ufunguzi rasmi wa Bunge Jipya utakaofanywa na
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania.
Aidha, inasisitizwa kwamba Wabunge Wateule wote
wafike wakiwa na nyaraka zifuatazo:-
(a)
Hati ya Kuchaguliwa/Kuteuliwa kwa Mbunge;
(b)
Nakala ya kitambulisho cha Taifa;
(c)
Kadi ya Benki yenye Namba ya Akaunti ya Mbunge;
(d)
Cheti cha Ndoa kinachotambuliwa na Serikali (Kwa
wenye Ndoa);
(e)
Cheti cha kuzaliwa cha Watoto wenye umri chini ya
miaka 18 (Kwa wenye Watoto);
(f)
Vyeti vya Elimu/Taaluma;
(g)
Nakala ya Wasifu wa Mbunge (Curriculum Vitae);
(h)
Picha (Passport size) nakala 8.
Imetolewa na: Katibu wa Bunge,
Ofisi ya
Bunge,
DODOMA.
7 Novemba,
2020
TUNALITAKIA BUNGE LETU KILA LA KHERI WANAPOANZA MAJUKUMU YAO YA KUTUWAKILISHA WATANZANIA. MWENYEEZI MUNGU AWABARIKI. AAAMIIIN.
ReplyDelete