Baadhi huruka angani, wengine huogelea baharini na wengine hukimbia ardhini kulingana na mtandao wa OneKindPlanet unaoangazia elimu ya wanyama.
10. Sungura wa Hudhurungi
Ana miguu mirefu ya rangi nyeusi inayomuwezesha kukimbia kwa kasi ya kilomita 77 kwa saa, kasi sawa na mbwa mwitu mwekundu.
9. Nyumbu wa Samawati
Nyumbu wa buluu, Springbok na gazelle wote wanaweza kukimbia kasi ya kilomita 80 kwa saa karibu sawa na kasi ya simba
8. Samaki aina ya Marlin
Marlin anaweza kuogelea kwa kasi ya kilomita 80 kwa saa, akinyang'anywa taji hivi karibuni na samaki aina ya Sail ambaye ndiye mwenye kasi zaidi duniani.
7. Paa wa Pembe la Kuchoma
Swala aina ya Pronghorn ni mnyama wa pili wa ardhini mwenye kasi ya kilomita 98 kwa saa.
6. Samaki wa Tanga
Samaki huyu ni mwenye kasi zaidi duniani, akiwa na kasi ndani ya maji ya kilomita 110 kwa saa.
5.Duma
Duma ana ujuzi katika kukimbia haraka na anaweza kufikia kasi ya kilomita 113 kwa saa.
Hiyo ni kasi kubwa mara tatu ya binadamu ambaye ana uwezi wa kukimbia kilomita takribani 36 kwa saa . Duma wana ujuzi kuliko mnyama mwingine wa aina yake.
4. Bata bukini- mwenye mabawa ya ncha
Bata bukini ni bata mkubwa duniani anayeweza kupaa kwa kasi ya kilomita 142 kwa saa.
3. Ndege Msindikizaji
Hukimbia umbali wa kilomita 153 kwa saa anasaidiwa na urefu wa mabawa yake ukioanisha na uzito wa mwili wa ndege yoyote. Ndege hawa wana uwezo wa kukaa angani kwa zaidi ya wiki moja.
2. Ndege aina ya Spine Tailed Swift
Ni ndege mwenye rangi nyeupe shingoni na mkia uliochongoka, ni ndege mwenye zaidi anapopaa akiwa na kasi ya kilomita 171 kwa saa.
1.Kipanga
Ndiye ndege mwenye kasi zaidi, kwa hakika ndiye mnyama aliye na kasi zaidi kwenye sayari, wakati akiwa kwenye mbizi ya uwindaji, huinuka kwa umbali mrefu, kisha huzama kwa kasi ya zaidi ya kilomita 322 kwa saa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇