LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 14, 2020

OKASH AWAONGOZA WANAWAKE KWENDA VILABU VYA POMBE KUZISAKA KURA ZA DK MAGUFULI

Mgombea Ubunge Viti  Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia CCM, Halima Okash (aliyeshika kipaza sauti) akielezea sera za CCM katika moja ya vilabu vya pombe katika Kata ya Nhinhi, Jimbo la Mvumi Dodoma, ambapo aliwaongoza wanawake hapo kuwaombea kura Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli, Mgombea Ubunge Jimbo la Mvumi, Livingstone Lusinde na Mgombea Udiwani wa Kata ya hiyo, Msafiri Mdandalu.
Okash akiwa katika kikao na wanawake kabla ya kuwashswishi kwenda nao kwenye vilabu vya pombe kuwaombea kura wagombea wa CCM.
Akina mama wakisikiliza kwa makini wakati Okash akimwaga sera za CCM.

Okash akiwaongoza kwenye vilabu vya pombe kufanya kampeni za CCM.



Na Mwandishi Wetu, Mvumi.
MGOMBEA Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia CCM, Halima Okash amewaongoza wanawake kwenda vilabu vya pombe kumuombe kura Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli.

Tukio hilo la kijasiri alilifanya baada ya kikao cha  ndani na wanawake hivi karibuni katika Kata ya Nhinhi Jimbo la Mvumi, Dodoma. Anasema kilichomsukuma kuchukua uamuzi huo ni baada ya kuona asilimia kubwa ya wanaume hawahudhurii mikutano ya kampeni.

Walipofika kwenye vilabu vya pombe ambapo asilimia kubwa wanywaji walikuwa wanaume vijana kwa wazee, Okash aliwasalimia kwa heshima za kimila na desturi za kiafrika na kuanza kumuombea kura Dk. Magufuli, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mvumi, Livingstone Lusinde na Mgombea Udiwani wa kata hiyo, Msafiri Mdandalu.

Alitumia fursa hiyo kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi kwa kuelezea mambo mazuri yaliyomo humo kuhusu yatakayotekelezwa katika jimbo la Mvumi, Mkoa wa Dodoma na jinsi wazee watakavyosaidiwa, vijana kupata mikopo yenye riba nafuu ambapo pia wanawake na walemavu wataipata.

Okash, aliomba kura kwa kuwaeleza mafanikio makubwa yaliyofanywa na Seikali ya CCM ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Jemadari Dk. Magufuli ambaye ndiye Mgombea Urais wa Tanzania. 

"Rais Magufuli ametuthamini mno wanaDodoma kwanza kuamua kuishi na sisi, kutupa hadhi kuwa makao makuu ya nchi, kuimarisha miundombinu ya barabara, nishati ya umeme hadi vijijini, ujenzi wa Stendi kubwa ya mabasi, soko la kisasa la Job Ndugai, hivyo tusimwangushe kinachotakiwa ni kumpigia kura nyingi Oktoba 28," alisema Okash uhuku akipigiwa makofi ikiwa ni ishara kuwa wamekubali.

Okash aliendelea kuwatajia miradi mbalimbali iliyotekelezwa na itakayotekelezwa katika Mkoa wa Dodoma kuwa ni; Ujenzi wa Barabara ya pete (Ringroad) yenye urefu wa zaidi ya Km 100 kuzunguka Jiji la Dodoma, ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato na hivi karibuni Dk. Magufuli ametangaza kujengwa kwa uwanja mkubwa wa michezo utakaoingiza watazamaji 80,000, Reli ya kisasa ya SGR Nk.

katika mikutano hiyo ya ndani na vilabuni, Okash  anawaasa wananchi kuacha kusikiliza propaganda za uongo zinazotolewa na wagombea wa upinzani katika mikutano yao ya kampeni, bali wasikilize sera nzuri na mipango mizuri ya kimaendeleo inayofanywa na Serikali ya CCM ambayo kila mmoja anaiona kwa macho.

"Ili kuwakomesha wapinzani kwa uongo wao na mipango yao ya kufukirika, hakuna adhabu nyingine ya kuwapa bali ni kuwanyima kura siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, 2020,"alisema Okash huku akishangiliwa.

 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages