LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 14, 2020

MOTO WA KAMPENI ZA CCM ULIVYOWAKA KATIKA JIMBO LA KAWE MBELE YA MGOMBEA URAIS WA CCM DK. MAGUFULI, LEO

Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akisakata muziki wa Singeli baada ya kuitwa jukwaani na msanii wa muziki huo, wakati wa mkutano wa kukataka na shoka, wa kampeni za CCM uliofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam,ukiongozwa na Mgombea Urais wa CCM Dk. John Magufuli, leo.👇





Wananchi wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally aliposakata muziki huo wa Singeli jukwaani wakati wa mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini dar es Salaam, leo
Vijana wa kundi la magufuli Gang, wakishambulia jukwaa wakati wa Mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam
Baadhi ya maelfu ya wananchi waliokuwa kwenye mkutano wa akampeni za CCM uliofanyika leo katika Viwanja vya Tanganyika Packers kawe jijini Dar es Salaam
Mwanamuziki wa muizki wa kizazi kipya Chege Chigunda akichangamsha hadhira kwenye mkutano huo
Mwanadada Shilole akiimba jukwaani na kuomba kura kwa CCM kwa mgombea urais wa CCM Dk. John Magufuli, Wabunge na Madiwani kwenye mkutano huo
Baadhi ya maelfu ya wananchi waliokuwa kwenye mkutano wa akampeni za CCM uliofanyika leo katika Viwanja vya Tanganyika Packers kawe jijini Dar es Salaam

Wagombea Ubunge na wagombea Udiwani katika majimbo na kata  mbalimbali mkoani Dar es Salaam wakijimwayamwaya kwa furaha wakati wa mkutano huo
Msanii wa muziki wa Singeli akichachafya kwa kutoa burudani jukwaani wakati wa mkutano huo
Msanii wa muziki wa singeli akionyesha umahiri wake wa kusakata muziki huo jukwaani wakati wa mkutano huo
Wagombea Ubunge na wagombea Udiwani katika majimbo na kata  mbalimbali mkoani Dar es Salaam wakijimwayamwaya kwa furaha wakati wa mkutano huo
Wagombea Ubunge na wagombea Udiwani katika majimbo na kata  mbalimbali mkoani Dar es Salaam wakijimwayamwaya kwa furaha wakati wa mkutano huo
Baadhi ya wagombea Ubunge na wagombea Udiwani katika majimbo na kata  mbalimbali mkoani Dar es Salaam wakimfurahia mwanamuziki wa muziki wa singenli aliyekuwa akitoa burudani katika mkutano huo
Chopa ya CCM ikipita anga la viwanja vya Tanganyika Packers kuongeza hamasa kabla mgombea Urais wa CCM Dk. John Magufuli hajawasili uwanjani
Kundi la Tanzania One Thetre (TOT) likitumbuiza mda mfupi kabla ya mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk. Magufuli kuwasili Uwanjani. Kulia ni Jerry John Komba, Kulia mtoto wa muasisi wa kundi hilo la TOT Marehemu Kapten John Komba
Msanii Nguli wa TOT Khadija Kopa akifanya mavituz yake jukwaani mda mfupi kabla ya Mgombea Urais wa CCM Dk. Magufuli kuwasili Uwanjani
Wacheza Shoo wa TOT wakiwajibika kuhamasisha kadamnasi wakati wa mkutano huo
Mwanadada Zuchu akiimba wimbo wake wa Regae wa 'Tanzania ya sasa" wakati Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk. Magufuli akiwasili Uwanjani
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Magufuli akiwapungia mkono wananchi alipowasili katika Uwanja wa Tanganyika Packers Kawe, kufanya mkutano mkubwa wa kampeni ambao ulikuwa wa mwisho kwa mkoa wa Dar es Salaam na pia wa kuzindua awamu ya sita na ya mwisho wa kampeni za CCM
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Magufuli akimsalimia Mgombea Ubunge jimbo la Kawe askofu Dk. Josephat Gwajima baada ya kuwasili kwenye mkutano huo
Wananchi wakimshangilia Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Magufuli alipowasili Uwanjani
Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam Sheik Alhad, akifanya maombi kuruhusu mkutano huo kuanza rasmi
Askofu Mwakibolwa akifanya maombi kuruhusu mkutano huo kuanza rasmi
Wananchi wakipokea maombi ya Askofu Mwakibolwa
Mchungaji Mwamposa akifanya maombi kuruhusu mkutano huo wa kampeni za CCM kuanza
TOT wakimwaga burudani

Mwanamuziki wa Muiziki wa kizazi kipya Harmonise akiimba wimbo la kuienzi CCM na Mgombea wake wa Urais Dk. John Magufuli. Awali aliimba akiwa amevaa shati lakini baada ya mzuka kupanda akaivua.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Kawe Askofu Dk. Josephat Gwajima akiomba kura za Rais, za kwake na za Madiwani katika jimbo la Kawe katika mkutano huo.

Msanii wa muziki wa kizazi Kipya Ali Kiba akiimba na kucheza na mgombea Udiwani Kata ya Kivukoni Sharik Choughle wakati wa mkutano huo👇

MWISHOOOO.  #Magufuli Mi 5, tena , Kazi Iendelee

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages