Manchester United imepewa tumaini kwamba inaweza kusaini mkataba na winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 20, baada ya 'kumuhukumu vibaya' alipomtaka msimu uliopita. (Star)
United pia wanamlenga kiungo wa kati wa Sporting Lisbon mwenye umri wa miaka 16-Luis Gomes. Kiungo huyo wa safu ya kati Mreno amepewa jina la ' Luis Figo' ajaye nchini mwake. (Mirror)
Winga wa Wolves Adama Traore, 24, yuko tayari kupokea wito Barcelona na Liverpool ili kusaini mkataba mpya wa pauni 100,000-kwa wiki katika Molineux.
Mshambuliaji huyo wa Uhispania alijiunga na klabu akitokea Middlesbrough mwaka 2018. (Sun)
Mlinzi wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher anasema klabu hiyo lazima imsaini kiungo wa safu ya kati-nyuma baada ya mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Virgil van Dijk, 29, kupata majeraha wakati wa mechi yao dhidi ya Everton. (Mail)
Winga wa Liverpool Harvey Elliott, mwenye umri wa miaka 17, alikitathmini kikosi cha Blackburn kabla ya kukubali uhamisho wa mkataba wa deni katika upande wa Championi.(Mail)
Mchezaji na kocha wa Derby County Wayne Rooney, mwenye umri wa miaka 34, anatarajia kupata matokeo ya vipimo vya Covid-19 test Jumatatu baada ya kugundua kuwa rafiki yake aliyemuuzia saa ya mkononi alikuwa na virusi vya corona. (Daily Telegraph - subscription required)
Klabu za EFL zinatishia kuzuwia jaribio la kulipa ushuru ili kupata dhamana ya serikali . (Sun)
Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, mwenye umri wa miaka 26, alikuwa na malumbano na afisa mkuu wa soka wa Juventus Fabio Paratici baada ya kuachwa nje ya kikosi kilichoingia uwanjani Jumamosi. (Mail via Tuttosport)
kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, pia analengwa na Barcelona. Mchezaji huyo, 29, yuko mwaka wa mwisho wa mkataba wake na msimu ujao atakuwa huru. (AD, via Sky Sports)
Winga Mfaransa Allan Saint-Maximin, mwenye umri wa miaka 23, alikuwa mmoja wa wachezaji wa Newcastle wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi aliposaini mkataba mpya wa miezi sita- ambapo malipo yake yaliongezeka mara dufu hadi kufikia pauni 70,000 kwa wiki. (Newcastle Chronicle)
Kocha wa West Ham David Moyes anasema alikuwa na helikopta tayari kumchukua juu kwa juu Gareth Bale aliyetoka Tottenham na kuelekea Real Madrid mwaka 2013 wakati huo akiwa kocha wa Manchester United. Mshambuliaji huyo wa Wales, 31, hivi karibuni alirejea Spurs kwa mkopo. (Mail)
Msambuliaji wa Manchester United na England Marcus Rashford, 22, amesema siku ya mwisho ya kuwasili kwa mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 33, kutasidia klabu hiyo kushindania kombe. (Sky Sports)
Kampuni iliyochukuliwa na Ligi ya Primia kuchunguza wachezaji ikiwa wana virusi vya corona imeunda vituo ambapo mashabiki watafanyiwa vipimo kwa dakika 15 kujaribu kuharakisha hatua ya kurejelewa kwa michuano kama kawaida. (Daily Telegraph - subscription required)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇