LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 19, 2020

HAFLA YA MAHAFALI NA SIKU YA WAZAZI ATLAS SCHOOLS YAFANA, DC CHONGOLO AINOGESHA

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godfrey Chongolo akimpongeza mhitimu wa Kidato cha Nne katika Atlas Schools Latifa Gumbo kwa kuibuka mshindi wa jumla baada ya kuongoza masomo matano ya Civics, Maths, English, Biology, na Chemistry dhidi ya wanafunzi wenzake. Chongolo alikuwa akigawa vyeti kwa wahitimu wa Kidato cha Nne, Msingi na Chekechea, wakati wa hafla ya mahafali na Siku ya wazazi ya Atlas Schools iliyofanyika jana kwenye kampasi ya shule hizo iliyopo Madale jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Schools Sylivanus Rugambwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godfrey Chongolo (kushoto) akiwa na mwenyeji wake Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Schools Sylivanus Rugambwa wakati akienda eneo la tukio baada ya kuwasili shuleni hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godfrey Chongolo (kushoto) akiwa na mwenyeji wake Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Schools Sylivanus Rugambwa wakati akienda eneo la tukio baada ya kuwasili shuleni hapo. Watatu kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Atlas Schools Johnson Kapira.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godfrey Chongolo akiwa tayari meza kuu kuendesha mahafali hayo
Mjumbe wa Bodi ya Atlas School Johson Kapira akitoa maneno ya utangulizi na kufungua rasmi hafla ya mahafali hayo na siku ya Wazazi (Atlay Day).

UZINDUZI WA DARAJA LA WANANCHI LILIJENGWA NA ATLAS SCHOOLS👇
Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Schools Sylivanus Rugambwa (kulia) akimwongoza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godfrey Chongolo kwenda kuzindua daraja la wananchi lilijengwa na Atlas School jirani kidogo na Taasisi hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Atlas Schools Johnson Kapira
Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Schools Sylivanus Rugambwa (kulia) akimuonesha hali ya mazingira Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godfrey Chongolo kabla ya kuzindua daraja hilo la wananchi lilijengwa na Atlas School jirani kidogo na Taasisi hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godfrey Chongolo akizindua daraja hilo huku akisaidiwa na Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Schools Sylivanus Rugambwa.
"Daraja hili la Wananchi limezindiliwa na Mkuu wa wilaya ya Kindondoni Godfrey Chongolo, Agosti 18, 2020", wakifurahia baada ya kusoma ujumbe kwenye jiwe la uzinduzi. Kisha Chongolo akasema, "Hongereni sana Atlas Schools, mmefanya kazi nzuri ya kusaidia jamii, nitawaambia watu wangu wawaandikieni barua ya shukrani na pongezi".
Baada ya kuzindua daraja hilo la wananchi wakapiga picha ya kumbukumbu ya pamoja
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godfrey Chongolo na Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Schools wakiondoka baada ya uzinduzi wa daraja hilo la wananchi na kurejea eneo la hafla ya mahafali
Mkuu wa Wilaya meza kuu yote na watu wote waliokuwa kwenye hafla hiyo wakiwa wamesimama wakati wananfunzi wa shule hiyo walipokuwa wakiimba wimbo wa Taifa na wimbo wa Atlas Schools.

Wanafunzi wakiimba wimbo wa Taifa na Wimbo wa Atlas Schools
Wanafunzi wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa
Wazazi wakiwa kwenye hafla hiyo
Wanafunzi wa shule ya msingi Atlas wakitumbuiza kwa ngonjera

----------

Wanafunzi wa Chekechea wa Atlas Schools wakiimba đź‘‡




------------

Wahitimu wa Darasa la Saba wakicheza muziki👇



Wahitimu wa Kidato cha Nne wakijinafasi kucheza muziki👇


---------------
Wanafunzi wakizungumza kwa niaba ya wanafunzi wote wa Atlas Schools wakati wa hafla hiyo.
Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas School Sylivanus Rugambwa akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godfrey Chongolo kuzungumza katika hafla hiyo. Kulia ni mama Rugambwa, mke wa Mkurugenzi huyo
Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Schools Sylivanus Rugambwa akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godfrey Chongolo kuzungumza katika hafla hiyo. Kushoto ni mama Rugambwa, mke wa Mkurugnzi huyo
Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Schools Sylivanus Rugambwa akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godfrey Chongolo kuzungumza katika hafla hiyo. Kushoto ni mama Rugambwa, mke wa Mkurugnzi huyo


Mkurugenzi Mtendaji wa Atlass Schools akimkaribisha jukwaani Mkuu wa Wilaya ya ya Kinondoni Godfrey Chongolo azungumze na hadhara
"Lakini kabla hajazungumza hapa tuna zawadi tulizomwandalia, medani ya mbio tulizofanya asubuhi na ngao ya kumbukumbu ya ujio wake hapa", akasema Mkurugenzi Mtendaji wa Atlass Schools wakati akimkaribisha jukwaani Mkuu wa Wilaya ya ya Kinondoni Godfrey Chongolo azungumze na hadhara
hapa nanakabidhiwa ngao hiyo
☝Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godfrey Chongolo akizungumza katika hafla hiyo👇

Wazazi katika hafla hiyo wakimsikiliza Chongolo

UTOAJI VYETI👇
Kidato cha nne wakiwa na vyeti vyao baada ya kutunukiwa na Mkuu wa Wilaya Daniel Chongolo
Mkuu Msaidizi wa shule hiyo akitangaza wanafunzi waliofanya vizuri zaidi
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godfrey Chongolo akimpongeza mhitimu wa Kidato cha Nne katika Atlas Schools Latifa Gumbo kwa kuibuka mshindi wa jumla baada ya kuongoza masomo matano ya Civics, Maths, English, Biology, na Chemistry dhidi ya wanafunzi wenzake. Kulia ni Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Schools Sylivanus Rugambwa.
Mhitimu wa Kidato cha Nne katika Atlas Schools Latifa Gumbo akionyesha vyeti alivyotuzwa kwa kuibuka mshindi wa jumla baada ya kuongoza masomo matano ya Civics, Maths, English, Biology, na Chemistry dhidi ya wanafunzi wenzake.
Kidato cha nne wakishuka jukwaani baada ya kutunikwa vyeti vyao
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godfrey Chongolo akibadilishana mawazo na Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Schools wakati wa mahafali hayo
Wahitimu Darasa la saba wakiwa na vyeti vyao
Wahitimu wa darasa la saba wakifurahi baada ya kutunukiwa vyeti vya kuhitimu
Chongolo akiwatunuku vyeti Chekechea
Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji akizungumza jambo




☝Chekechea wakifurahia kupata vyeti vyao vya kuhitimu

---------

WASHINDI WA MBIO ZA KM 5, 10 NA 21 WAKIZAWADIWA👇





------

NENO LA SHUKRANI 👇
Mjumbe wa Bodi ya Atlas School Johson Kapira akitoa maneno ya shukrani kwa mgeni rasmi mwishoni mwa  hafla hiyo ya mahafali hayo na siku ya Wazazi (Atlay Day). Kulia ni Philbert Komu ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Atlas Schools ambaye kwenye hafla hiyo alikuwa ndiye mwongoza shughuli (MC) 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godfrey Chongolo akisindikizwa na Mwenyeki wake, Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Schools Sylivanus Rugambwa wakati akiondoka mwishoni mwa hafla hiyo
Chongolo akiagana na baadhi ya viongozi wa Atlas School kabla ya kuondoka. Anayeagana naye ni Mjumbe wa Bodi ya Atlass Scools Johnson Kapira na katikati yao ni MMiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa  Atlas Schools Sylivanus Rugambwa
Viongozi na walimu wa Atlas Schools wakiendelea kumuaga Chongolo
"Haya kwaherini, mbaki salama na ninawatakia mwendelee na kazi njema ya kulijenga taifa", akasema Chongolo dakika chache kabla ya kuondoka. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO,  CCM Blog
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages