Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kufungua rasmi wa kiwanda cha kisasa cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro International Leather Industries Company Limited eneo la Karanga mjini Moshi leo Alhamisi Oktoba 22, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akiwa jukwaa kuu na viongozi wengine wakati wa Ufunguzi rasmi wa kiwanda cha kisasa cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro International Leather Industries Company Limited eneo
la Karanga mjini Moshi leo Alhamisi Oktoba 22, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza Suleiman Mzee pamoja na viongozi wa dini wakati akielekea kufungua rasmi kiwanda cha kisasa
cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro International Leather Industries Company Limited eneo la Karanga mjini Moshi leo Alhamisi Oktoba 22, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza Suleiman Mzee pamoja na viongozi wa dini wakati wakipata maelezo. ya kiwanda cha kisasa cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro International Leather Industries Company Limited kabla ya kukifungua rasmi eneo la Karanga mjini Moshi leo Alhamisi Oktoba 22, 2020Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akifunua pazia kufungua rasmi kiwanda cha kisasa cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro International Leather Industries Company Limited kabla ya kukifungua rasmi eneo la Karanga mjini Moshi leo Alhamisi Oktoba 22, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akikata utepe kufungua rasmi kiwanda cha kisasa cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro International Leather Industries Company Limited kabla ya kukifungua rasmi eneo la Karanga mjini Moshi leo Alhamisi Oktoba 22, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akikagua
bidhaa za. viatu baada ya kufungua rasmi kiwanda cha kisasa cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro International Leather Industries Company Limited kabla ya kukifungua rasmi eneo la Karanga mjini Moshi leo Alhamisi Oktoba 22, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akifurahia zawadi ya viatu alivyokabidhiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza Suleiman Mzee (kushoto) baada ya kufungua rasmi
kiwanda cha kisasa cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro International Leather Industries Company Limited kabla ya kukifungua rasmi eneo la
Karanga mjini Moshi leo Alhamisi Oktoba 22, 2020
PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 22 Oktoba, 2020 amezindua kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro (Kilimanjaro International Leather Industries Co. Ltd) kilichojengwa katika eneo la Gereza Kuu la Karanga, Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa ubia wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF) na Jeshi la Magereza Tanzania.
Mradi
wa ujenzi wa kiwanda hicho umehusisha uboreshaji wa kiwanda cha zamani
kilichojengwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere mwaka 1978 kwa
ajili ya kuzalisha viatu vya kijeshi ambapo kilikuwa kikizalisha jozi 150 kwa
siku, na sasa kimeboreshwa na kuongeza uzalishaji hadi kufikia viatu 400 kwa
siku.
Kiwanda
kipya na cha teknolojia ya kisasa kilichowekezwa hivi sasa na ambacho kimeanza
uzalishaji kina uwezo wa kuzalisha jozi Milioni 1.2 za viatu kwa mwaka, soli za
viatu jozi milioni 2.1 kwa mwaka pamoja na bidhaa mbalimbali za Ngozi kama vile
mikanda, mabegi, pochi na makoti, na pia kitakuwa na uwezo wa kuchakata futi
Milioni 13 za ngozi ambazo kwa asilimia 60 zitatumika kiwandani hapo na
asilimia 40 kuuzwa ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi
Mkuu wa PSSSF Bw. Hosea Kashimba amesema uwekezaji wa kiwanda hicho umegharimu
shilingi Bilioni 136, kinatarajiwa kutoa ajira takribani 3,000 za moja kwa na 7,000
zisizo za moja kwa moja, na kwamba katika kujihakikishia upatikanaji wa
malighafi za uhakika PSSSF inashirikiana na wadau wengine kuwekeza katika
machinjio ya kisasa nchini ili kupata ngozi bora za kukilisha kiwanda hicho.
Baada
ya kuzindua kiwanda hicho, Mhe. Rais Magufuli amejionea jinsi vijana wa
Kitanzania wanavyofanya kazi kwa kutumia mitambo ya kisasa ya kutengeneza viatu
bora vya aina mbalimbali na pia amenunua jozi kadhaa za viatu vilivyokuwa
tayari kwa kuuzwa.
Akizungumza
na wananchi waliohudhuria tukio hilo, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa
kwake na kukamilika kwa kiwanda hicho ambacho kimeboreshwa na kuwekezwa mitambo
na majengo mapya kwa maelekezo yake, na amesema anaamini uzalishaji wake
utaendelea kupanuliwa ili kupunguza matumizi makubwa ya fedha za kigeni
zinazotumika kuagiza viatu nje ya nchi ambapo takwimu zinaonesha Tanzania
inaagiza jozi Milioni 52 za viatu kwa mwaka.
Mhe.
Rais Magufuli amesema pamoja na ajira za moja kwa moja zitakazozalishwa na
kiwanda hicho, ajira nyingine takribani Milioni 3 zitazalishwa kutokana na
mnyororo wa thamani, soko la ngozi litapanuliwa na hivyo ametoa wito kwa wafugaji
kuzalisha ngozi bora.
Ameipongeza
PSSSF yenye asilimia 86 ya hisa za kiwanda hicho na Jeshi la Magereza kwa
kufanikisha uwekezaji huo, na ametoa wito kwa mifuko ya hifadhi ya jamii na
wadau wengine kuendelea kuwekeza katika viwanda kama ambavyo wamefanya katika
miaka mitano iliyopita ambapo Tanzania imefanikiwa kujenga viwanda vipya 8,470.
Mhe.
Rais Magufuli amewataka Watanzania wote kuendelea kudumisha amani ambayo ni
muhimu kwa maendeleo ya viwanda, hasa wakati huu ambapo Tanzania imeingia
katika uchumi wa kati, na amesisitiza kuwa Serikali itahakikisha inaendelea
kujenga mazingira bora ya uwekezaji ili Watanzania wanufaike.
Sherehe
ya uzinduzi wa kiwanda hicho imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Mhe. Jenister Mhagama, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George
Simbachawene, Kamishna Jenerali wa Magereza Suleiman Mzee, Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Bi. Anna Mghwira, viongozi wa Dini, viongozi na watendaji wakuu wa
mifuko ya hifadhi ya jamii.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇