Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MABINGWA watetezi, Simba SC leo wamepoteza mechi ya kwanza ya msimu katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuchapwa bao 1-0 na wenyeji Tanzania Prisons, Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.
MABINGWA watetezi, Simba SC leo wamepoteza mechi ya kwanza ya msimu katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuchapwa bao 1-0 na wenyeji Tanzania Prisons, Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.
Simba SC, mabingwa mara tatu mfululizo wa Ligi Kuu, wanabaki na pointi zao 13 baada ya kipigo cha leo, sasa wakizidiwa pointi tatu na mahasimu wao, Yanga SC baada ya timu zote kucheza mechi sita, wakati Azam FC wanaendelea kuongoza kwa pointi zao 21 za mechi saba.
Bao lililoizamisha Simba SC inayofundishwa na Mbelgiji, Sven Ludwig Vandenbroeck limefungwa na mshambuliaji Samson Mbaraka Mbangula dakika ya 49 akimalizia kazi nzuri ya beki Michael Ismail Mpesa.
Ushindi wa leo kwa Tanzania Prisons unawafanya wafikishe pointi tisa baada ya kucheza mechi saba na wanapanda kutoka nafasi ya 14 hadi ya tisa kwenye Ligi Kuu ya timu 18.
Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Yanga SC wameichapa 1-0 Polisi Tanzania bao pekee la kiungo Mkongo, Mukoko Tonombe dakika ya 70 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Tanzania Prisons kilikuwa; Jeremiah Kisubi, Michael Mpesa, Benjamin Asukile, Vedastus Mwihambi, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil, Salum Kimenya/Adili Buha dk58, Ezekia Mwashilindi, Samson Mbangula, Jeremiah Juma/Ramadhan Ibata dk81 na Lambert Sibiyanka.
Simba SC; Aishi Manula, Shomari Kapombe/Kennedy Wilson dk14, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Joash Onyango, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Hassan Dilunga/Muzamil Yassin dk73, Rally Bwalya, Charles Ilamfya/Miraj Athumani ‘Madenge’ dk62, Luis Miquissone na Bernard Morrison.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇