Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF, Christopher Mapunda akielezea utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya NHIF, mafanikio na utatuzi wa changamoto mbalimbali kuelekea maadhimisho ya miaka 20 ya mfuko huo. |
Mhariri wa Kituo cha Televisheni/Radio CLOUDS, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Joyce Shebe akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wahariri wakati wa mkutano huo. |
Meneja Uhusiano wa NHIF, Joyce Mziray akiongoza mkutano huo. |
Leonard Mwakalebela wa Gazeti la Daily News,
Na Richard Mwaikenda.
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga amewaomba wahariri wa vyombo vya habari nchini, kuunga mkono agenda ya serikali kuwa na muswada wa kutungwa kwa sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.
Ombi hilo alilitoa wakati wa mkutano wa tano na wahariri wa vyombo vya habari nchini uliofanyika Oktoba 22, 2020 jijini Dodoma.
Konga alisema vyombo vya habari ni muhimu sana katika kuelimisha jamii, hivyo ametaka uwepo ushirikiano kuhakikisha suala hilo linafanikiwa kwa kiwango kikubwa ili watanzania wote wawe na Bima ya Afya.
Pia amewasihi wahariri kushiriki kutoa maoni na ushauri wa kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wanachama na Umma kwa ujumla, Kuendelea kuwa mabalozi wa Mfuko kupitia Taaluma zao.
Wameshauriwa kutumia Ofisi za Mfuko zaidi ya 30 katika mikoa ili kutatua changamoto zinazojitokeza kwa wanachama, lakini pia kujenga ushirikiano na Mfuko katika kutoa elimu kwa wanachama na umma kwa ujumla kuhusu dhana na umuhimu wa bima ya afya.
Katika mkutano huo uliofunguliwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bernard Mbanga, wahariri wameshiriki majadiliano na kutoa ushauri mbalimbali jinsi ya kuboresha huduma za mfuko huo ambao mwakani unaadhimisha mika 20 tangu uanzishwe rasmi 2001.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇