LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 14, 2020

PROFESA KABUDI APATA AJALI MOROGORO

Profesa Kabudi
Morogoro, Leo

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, amelazwa Hopstali baada ya kupata ajali mkoani Morogoro, leo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare amethibitisha kutokea ajali hiyo.

Amesema Profesa Kabudi alipata ajali hiyo njia ya kwenda Dodoma nje kidogo ya Mji wa Morogoro akiwa safari kwenda jimboni kwake Kilosa.

Mkuu huyo wa mkoa amesema na yeye alikuwa kwenye msafara huo, lakini alikuwa amemtangulia na ndipo walipigiwa simu kwamba Waziri amepata ajali, hivyo ilibidi warudi Morogoro na walikuta tayari ameishafikishwa hospitalini.

Amesema alipata bahati ya kumuona anaendelea vizuri, huku madaktari akiendelea kumhudumia na kwamba hana tatizo kubwa sana.

Mkuu huyo wa mkoa amewatoa wasiwasi Watanzania na wananchi wa Kilosa kwamba anaendelea vizuri na baadaye watasikia madaktari watakavyowashauri.

Chanzo cha habari hii: TimesMajira Online

2 comments:

  1. Tuendelee kumwombea afya yake izidi kuimalika zaidi ili aweze kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa hili haraka ipasavyo🙏

    ReplyDelete

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages