LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 14, 2020

KATIBU MKUU WA CCM KUKUTANA NA MABALOZI WANAOZIWAKILISHA NCHI ZAO HAPA NCHINI, KESHO

Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally

CCM Lumumba, Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ally Kakurwa, kesho anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.


Taarifa iliyotolewa na Afisa habari wa Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM Said Said Nguya, imesema mazungumzo hayo yatafanyika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam kuanzia mida ya saa nne asubuhi.


Said amesema vyombo mbalimbali vya habari vinaalikwa kufuatilia kwa minajili ya kuhabarisha Umma kuhusiana na mazungumzo hayo.

2 comments:

  1. Kidumu chama Cha mapinduzi,sawa mkuu ongea nao hao mabalozi,uwaambie wafanye kilicho waleta na si kuchunguzachunguza mambo yetu hayawahusu,waambie pia kuwa sisi Ni taifa huru tunao wajibu wakufanya chochote tunachotaka maadamu hatuvunji Sheria za kimataifa,ujumbe huu unawahusu mabalozi wa nchi za kibepari.

    ReplyDelete

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages