LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 13, 2020

OKASH: KUUPIGIA KURA UPINZANI NI SAWA NA KUONJA SUMU, IPIGIENI CCM MPATE FARAJA



Okash akielezea yaliyomo kwenye Ilani ya CCM ya Uchaguzi kuhusu yajayo yatakayotekelezwa na Serikali ya CCM endapo itapigiwa kura na kushinda.
Okash akimnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Loje, John Njooka.
Wananchi wakishangilia  baada kufurahishwa na jinsi Okash alivyokuwa akielezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. John Magufuli.
Wanawake wakimsikiliza kwa makini Okash alipokuwa akielezea mikakati mbalimbali ya ushindi kwa wagombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28.Pia aliwaomba kuwa mabalozi katika kuzisaka kura hizo hata kwa watu wengine.
Okash akiwa katika mkutano wa ndani wa kampeni za CCM katika Kata ya Mlowa Jimbo la Mvumi ambapo alizungumza na wanawake na kuwaombea kura wagombea wa CCM.

 Okash akimnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Mlowa Bwawani, Andrew Msea.



Na Mwandishi Wetu, Mvumi.

WANAWAKE wameaswa kutodanganyika na wapinzani kwani katika majimbo waliyokuwa wanayaongoza hakuna walilofanya la maendeleo na kwamba hata wakipewa nchi hawawezi kutekeleza kama alivyofanya mambo makubwa Rais John Magufuli na Serikali yake ya Chama Cha Mapinduzi.

Wametahadharishwa kutothubutu hata chembe  Oktoba 28  kwenda kuwapigia kura wapinzani kwani kufanya hivyo ni sawa na kujaribu kuonja sumu unapotaka kuinunua, jambo ambalo ni hatari.

Kauli hiyo imetolewa na Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia CCM, Halima Okash katika Kata ya Loje Jimbo la Mvumi, Dodoma, alipokuwa akimuombea kura Mgombea Udiwani wa Kata hiyo, John Njooka, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mvumi, Livingstone Lusinde na Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli.

Alisema kuwa mifano halisi ipo kwa viongozi na wabunge wa upinzani katika majimbo yao hakuna lolote la maana walilofanya hivyo kuendelea kuwapa mateso wananchi wa maeneo hayo.

"Ulizeni wenzenu walio kwenye majimbo yanaayoongozwa na upinzani, wanajuta huku wakilia na kusaga meno kwa shida na taabu wanazopata, wameapa hawatarudia tena kuwapigia wapinzani bali sasa wameahidi kuwapigia wagombea safi wa CCM.

Mlisikia wapi kwamba unaonja sumu kabla ya kuinunua? Kujaribu kuwapigia kura wapinzani ni sawa na kujaribu kuonja sumu, achana nao kabisa si watu wema, twendeni Oktoba 28 tukawapigie wagombea wa CCM mpate maendeleo, neema na faraja,"Okash aliwasihi akina mama.

Akiwa katika mkutano wa kampeni katika Kata ya Mlowa Jimboni humo, Okash aliinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi kwa kuelezea mipango mizuri ya maendeleo iliyomo humo, aliwakumbusha wanaDodoma kuwa mkoa huo sasa ndiyo uso wa nchi na kwamba maendeleo mengi yataanzia katika Jiji hilo ambalo ni makao makuu ya nchi.

"Ninawakumbusha wana Mvumi kuwa Dodoma ndiyo uso wa Nchi kwa sasa na kwamba maendeleo mengi yataanzia kwetu, hivyo tusimwangushe Rais wetu Dk John Magufuli  tumpe kura nyingi za kishindo ametuthamini mno wana Dodoma kwa kutupa makao makuu ya nchi na kutuletea maendeleo,"alisema Okash.

Alitaja baadhi ya mambo ambayo Mkoa wa Dodoma umenufaika wakati wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Dk. Magufuli kuwa ni; Dodoma kutangazwa kuwa Jiji, kuhamishia makao makuu ya nchi, Rais  kuhamia Ikulu ya Chamwino, Ujenzi wa Stendi ya Kisasa na Soko la Kisasa la Job Ndugai.

Miradi mingine ni;Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR, kuanza kwa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato na kuanza ujenzi wa barabara za pete (Ringroads) kulizunguka jiji la Dodoma na hivi karibuni JPM ametangaza kujenga Uwanja Mkubwa wa Kisasa wa michezo.

Okash amekuwa akifanya kampeni kabambe katika  kata mbalimbali katika majimbo ya Kondoa Vijijini na Jimbo la Mvumi ambapo kila mara amekuwa akihimiza siku ya Oktoba 28, wananchi kuwahi mapema na shahada zao kwenda kuwapigia kura wagombea wa CCM.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages