Mgombea Ubunge jimbo la Mchinga mkoani Lindi, Mama Salma Rashid Kikwete akinadiwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Japhari Kubecha Mghamba katika mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika katika Kata ya Marimba, jana.
Mchinga, Lindi
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Japhari Kubecha Mghamba ameshiriki kumnadi Mgombea Ubunge jimbo la Mchinga mkoani Lindi, Mama Salma Rashid Kikwete kwenye mikutano ya Hadhara iliyofanyika katika Kijiji cha Kitwaavi na Likwaya kwenye kata ya Marimba.
Katika mikutano hiyo ya kampeni za CCM, pamoja na kumuombea kura Mama Salma Kubecha alimuombea kura za kishindo Mgombea Urais wa CCM, Dk. John Magufuli na Wagombea Udiwani katika jimbo hilo la Mchinga.
Akiomba kura, Kubecha aliwaomba wananchi kumchagua rais Dk. Magufuli, Mama Salma na Madiwani wote katika kata hiyo, ili Chama Cha Mapinduzi kiweze kufanya kazi kwa uhakika katika kuwaletea maendele wananchi wa jimbo hilo la Mchinga katika awamu inayofuata.
" Wananchi nawasili sana na kuwaomba kwa unyenyekevu mkubwa Mchagueni Dk. John Magufuli kwa sababu ndiye mgombea pekee wa Urais ambaye amekwishaonyesha mfano wa kuliletra taifa letu maendeleo kwa kasi kubwa, na kwa kumchagua ninaamini aatafanaya kazi kubwa zaidi ya hii aliyokwishafanya", alisema Kubecha.
Akimuombea kura Mama Salma Kikwete, Kubecha aliwaomba wananchi wamchague kuwa mbunge wao kwa kwa sababu maendeleo maendeleo ambayo yametekelezwa katika awamu hii inayomaliza mda wake ametoa mchango mkubwa, hivyo wakimchagua ataendelea kutoa mchango mkubwa azaidi katika kuleta maendeleo katika jimbo la Mchinga na Taifa kwa jumla.
" Huyu Mama yetu, Mama Salma ameweza kuwasaidia vijana wengi hapa Mchinga kwa kuwasomesha na bado anaendelea kufanya hivyo nanyi ni mashahidi, hivyo mchagueni ili aweze kuendelea kuboresha zaidi suala la Elimu katika jimbo hili ili kuweza kuwasaidia vijana wengi kupata elimu kwa ajili ya kusaidia jamii zao", alisema Kubecha.
Akiomba kura, Mama Salma aliwaomba wananchi wa Jimbo la Mchinga kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kuwa amejipanga kutekeleza vyema ilani ya CCM 2020-25 katika jimbo hilo na pia atahakikisha Mchinga inakuwa mpya kwa kuweza kupata barabara na pia kunufaika kwa awamu ya tatu na mpango wa Umeme Vijijini (REA) na hali kadhalika kuhakikisha maeneo yote ya vijijini kuna kuwa na Zahanati na shule ili Mchinga iwe mpya zaidi kimaendeleo.
TAZAMA KATIKA PICHA TASWIRA YA KAMPENI HIZO 👇
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇