LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 24, 2020

OKASH AUNGANA NA SPIKA NDUGAI KUZISAKA KURA ZA DK. MAGUFULI KONGWA

Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Halima  Okash akimwaga sera za CCM  kwenye mkutano wa kampeni Kata ya Chamkoroma  Jimbo la Kongwa alipokwenda kuungana na Mbunge Mteule wa jimbo hilo, Spika Job Ndugai (kushoto) kuzisaka kura za Mgombea Urais wa CCM, Dk. John Magufuli.
Ndugai na Okash wakifurahia jambo wakat wa mkutano wa kampeni.
Ndugai na Okash wakijadiliana jambo wakati wa kampeni


Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na maneno mazuri ya kampeni ya Okash. 


Ndugai akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM, Dk Magufuli.
Okash akiomba kura za Dk. Magufuli kwa uneynyekevu.


Ni burani kwa kwend mbele katika mkutano wa kmpeni Jimbo la Kongwa.

Spika Ndugai akichez ngoma ya asili iliyokuwa kitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni.


Na Mwandishi Wetu, Kongwa.


MGOMBEA Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Halima  Okash ametinga Jimbo la Kongwa kuungana na Mbunge Mteule wa jimbo hilo, Spika Job Ndugai kuzisaka kura za Mgombea Urais wa CCM, Dk. John Magufuli.


Mama huyo mchakalikaji ambaye hadi sasa ameshafanya kampeni zaidi ya kata 70 mkoani Dodoma, amekwenda Kongwa mwishoni mwa wiki, kuungana na Spika Ndugai pamoja na viongozi wengine wa CCM kufanya kampeni za kumuombea kura Dk. Magufuli na wagombea wengine wa chama hicho. 


Kama kawaida yake Okash akiwa katika mikutano ya kampeni katika baadhi ya kata za Jimbo la Kongwa, ambako alipiga kambi ya siku tatu, aliomba kura za Dk. Magufuli kwa unyenyekevu huku akiwa amepiga magoti jambo ambalo lilisababisha apigiwe makofi na wananchi.


Okash na Spika Ndugai ambaye amepita bila kupingwa, walikwenda katika baadhi ya kata na vijiji, kuomba kura za Dk Magufuli na kuwashukuru kwa kumpitisha Ndugai bila kupingwa pamoja na baadhi ya wagombea udiwani wa chama hicho.


Akiwa katika mkutano wa kampeni katika Kata ya Iduo,vijiji vya Chang'ombe na Iduo, Okash aliwashukuru wananchi kwa imani yao ya kuwaamini na kuwapitisha bila kupingwa Spika Ndugai na mgombea udiwani wa kata hiyo. Zaidi ya Kata 17 wagombea udiwani wa CCM wamepita bila kupingwa. Zimebakia kata 5.


"Tunawashukuru sana wananchi kuwapitisha bila kupingwa Mgombea Udiwani wa Kata hii ya Iduo, Valentino Seng'unda na Mgombea Ubunge Jimbo la Kongwa, Ndugai na kwa imani hiyo mliyonayo kwa CCM tunaamini Jumatano Oktoba 28, hamtafanya makosa, mtampigia kura nyingi Dk. Magufuli,"alisema Okash huku akipigiwa makofi. 


Okash alikwenda pia katika vijiji vya Mseta na Manghweta Kata ya Chamkoroma ambapo katika mikutano ya kampeni alimuombea kura Dk. Magufuli kwa vile Mgombea  udiwani wa Kata hiyo,Simon Binde alipita bila kupingwa.


Akiwa katika Kata hiyo aliwasihi wananchi kumpigia kura Dk. Magufuli ili azidi kuwaletea maendeleo kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Aliwatahadharisha kutokuwa na ndoto wala mawazo ya kuupigia upinzani akidai hauna dira yoyote ya kuwaletea watanzania maendeleo.


Diwani Mteule wa Kata ya Chamkoroma, Simon Binde, alimmwagia sifa lukuki, Okash kwa mtindo wake wa kuomba kura kwa unyenyekevu akidai huyo mama ni jembe na ameiva hasa kisiasa.


"Aisee aliyoyafanya Okash yamenishangaza fikiria na urembo wake ameamua kupiga magoti kwenye udongo mwekundu kumuombea rais kura?!!! kweli huyu mama ni jembe kweli kweli, ni chachu na siasa anaijua, anajua kupangilia maneno yenye hamasa ya kumuombea kura Dk. Magufuli kiasi cha kuwafurahisha wanawake na wanaume. Yuko vizuri nina imani atafika mbali kisiasa," amesema Binde.


Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), wilaya ya Kongwa, Alpha Mwegalawa  aliyeambatana na Okash kwenye kampeni katika baadhi ya vijiji katika Kata za Chamkoroma na Iduo, anasema ndani ya siku tatu alizokuwa naye amefanya mambo makubwa, ameutumia muda wake mwingi kujikita kumuombea Dk Magufuli kura.


"Amefanya kampeni kiukweli ukweli, huyu mama ameiva kisiasa, ndani ya siku tatu amejitolea muda wake kisawasawa kumuombea kura Dk. Magufuli, akiwa jukwaani anaeleweka kwani anapangilia vizuri maneno, yaani hata akiongea sura yake inaonesha dhahiri anaomba kura si mzaha, Mungu ambariki afike mbali kisiasa," alimalizia kusema Mwegalawa.


 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages