Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Karatu kwenye uwanja wa Mnada wilayani karatu mkoani Arusha akiwa njiani kuelekea Karatu kwa ajili ya Mkutano wa Kampeni za CCM leo Jumamosi Oktoba 24, 2020.
Rais Dk. Magufuli amewaomba wananchi wa Karatu kubadilisha mwelekeo wa Karatu kwa kuchagua wagombea CCM ili kuleta maendeleo ya wilaya hiyo iliyosimama kwa muda mrefu katika maendeleo.
(PICHA NA JOHN BUKUKU)
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Ndugu Zelothe Steven akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli na kumkaribisha ili kuzungumza na wananchi kwenye uwanja wa Mnada.
Wagombea Udiwani wa jimbo la Karatu wakiserebeka na muziki wa kwaya ya Karatu iliyokuwa ikitumbuiza kwenye mkutano huo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli akifurahia kwaya ya Karatu wakati alipokuwa ikitumbuiza kwenye mkutano huo.
Baadhi ya viongozi wa dini mbalimbali wakishiriki katika mkutano huo kwa kuomba dua.
Baadhi ya viongozi wa chama cha Mapinduzi CCMwakishiriki katika mkutano huo.
Baadhi ya wana CCM wakisikiliza kwa makini wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia kwenye uwanja wa Mnada mjini Karatu.
Picha mbalimbali zikionesha maelfu ya wananchi waliofurika kwenye uwanja wa Mnada mjini Karatu ili kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati akiwaomba kura ili wamchague ifikapo Oktoba 28,2020.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇