LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 11, 2020

MAJALIWA: MAFUNDISHO YA DINI YANACHANGIA AMANI NA UTULIVU NCHINI

Na Mwandishi Maalum, Korogwe
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mafundisho ya dini ambayo yamekuwa yakitolewa na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini hapa nchini yametoa mchango mkubwa wa kuifanya Tanzania kuendelea kuwa nchi nzuri na yenye amani na utulivu duniani.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana, wakati akizindua Msikiti wa Rahman ambao umejengwa kwa gharama ya sh. milioni 150 kwa ufadhili wa taasisi ya Firdausi, katika Kijiji cha Kwamndolwa wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Waziri Mkuu amesema Viongozi hao wa dini hapa nchini wanatakiwa waendelee kuwarithisha watoto wote imani za dini  ili kuwajenga katika misingi mizuri ya maadili itakayowafanya wawe raia wema kwa kuwa na hofu ya Mungu mioyoni mwao.

Aliwashukuru viongozi wa dini nchini kwa kuliombea Taifa tangu mchakato wa uchaguzi mkuu ulipoanza akisema, “Tunawashukuru viongozi wa dini, tuna zaidi ya mwezi mmoja tangu kuanza kwa  kampeni na bado amani inaendelea kutawala nchini, hivyo msichoke kuliombea Taifa na kuwaombea wote wanaoshiriki katika mchakato wa kampeni.”
 
Ufunguzi huo umehudhuriwa na Mufti wa Tanzania Sheikh Mkuu Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Kasongwa, waumini wa Kiislam na wakazi wa Kwamndolwa kwa jumla.

Pamoja na Taasisi ya Firdaus kufadhili ujenzi wa Msikiti huo kwa gharama ya Sh. milioni 150  Taasisi hiyo pia  imekuwa ikijenge misikiti mbalimbali na kutoa misaada mingine ikiwemo kuchimba visima vya maji kwenye maeneo mbalimbali nchini.
------------------
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir bin Ally wakifungua Msikiti wa Rahmaan katika kijiji cha Kwamndolwa wilayani Korogwe, Oktoba 10, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir bin Ally wakati alipowasili  kwenye kijiji cha Kwamndolwa wilayani Korogwe kufungua Msikiti wa Rahmaan, Oktoba 10, 2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka ndani ya Msikiti wa Rahmaan katika kijiji cha Kwamndolwa wilayani Korogwe baada ya kuufungua Msikiti huo, Oktoba 10, 2020. Kulia kwake ni Mufti na Sheikh Mkuu waTanzania, Abubakar Zubeir bin Ally.
 
 Wananchi wa Korogwe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua Msikiti wa Rahmaan katika kijiji cha Kwamndolwa wilayani Korogwe, Oktoba 10, 2020.
 Wananchi wa Korogwe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua Msikiti wa Rahmaan katika kijiji cha Kwamndolwa wilayani Korogwe, Oktoba 10, 2020.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kufungua Msikiti wa Rahmaan katika kijiji cha Kwamndolwa wilayani Korogwe, Oktoba 10, 2020. Kushoto ni Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir bin Ally.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages