LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 11, 2020

DK. MAGUFULI KUFUNGA KAMPENI ZAKE KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM KWA KUUNGURUMA KATIKA JIMBO LA KAWE

CCM Lumumba, Dar es Salaam

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema mkutano wake mkubwa  wa kufunga kampeni katika Jiji la Dar es Salaam, utafanyika  siku ya Jumatano, Oktoba 14, 2020 katika Jimbo la Kawe, kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers ambako Mgombea wake wa Urais Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli ataunguruma vya kutosha kwenye viwanja hivyo.


Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kuhusu mwendelezo wa ratiba ya Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Rais Dk. John Magufuli katika Jijini la Dar es Salaa, imeeleza kwamaba mkutano huo wa Tanganyika Packers utaanza saa 3.00 asubuhi na amewakaribisha Wanachama wote wa CCM na wananchi wapenda maendeleo ya Dar es Salaam, kufika saa 2.00 asubuhi kabla ya mkutano huo kuanza rasmi. 


Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ratiba ya Mgombea huyo katika jiji la Dar es Salaam, itaanza kesho Oktoba 12, 2020, kwa mkutano mkubwa ambao utafanyika katika Jimbo la Segerea Wilayani Ilala, katika eneo la Kinyerezi Mwisho, Njiapanda ya kwenda Mitambo ya kufua umeme kwa gesi, ambapo Polepole amewakaribisha Wanachama wa CCM na wanannchi wote kwa jumla kufika mapema saa 2 asubuhi kabla ya mkutano huo kuanza saa 3:00 Asubuhi.


Polepole ameleza katika taarifa hiyo kwamba keshokutwa, Oktoba 13, 2020 utafanyika mkutano mwingine mkubwa Uwanja wa Mburahati Barafu katika Jimbo la Ubungo, Wilaya ya Ubungo ambako pia  wana CCM na Wananchi wote amewaomba kufika Uwanjani saa 1 asubuhi kabla ya mkutano kuanza 2 Asubuhi.


"Mikutano yote mitatu ratiba yake ina sehemu mbili, Sehemu ya kwanza ni Maelezo ya Utekelezaji wa Ilani ya 2015 – 2020 kutoka kwa wagombea ubunge wa CCM sambamba na kuomba kura, aidha sehemu hii ya kwanza inashereheshwa na vijana wana CCM wasanii wa muziki ambao pia watayaeleza mafaniko ya Awamu ya Tano kwa lugha ya Sanaa.


Sehemu ya pili itaongozwa na Ndugu Magufuli, mgombea wa nafasi ya Rais kwa tiketi ya CCM ambaye atatueleza tulikotoka, tuliko na tunakokwenda, itakuwa fursa ya kuyasikia maono yake kwa Dar es Salaam na Taifa", amesema Polepole katika taarifa hiyo na kuongeza;

 

"Taarifa ya ziada inatolewa kuwa siku ya tarehe 13 Oktoba 2020, Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atawaongoza Watanzania kupokea mgao wa zaidi ya Bilioni 100 kutoka Kampuni ya Barrick Gold ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya kupitia upya Mikataba ya Madini na kutunga sheria zinazolinda madini na maliasili za Tanzania".

TAARIFA KAMILI ILIYOTOLEWA NA NDUGU POLOEPOLE HIYO HAPO👇


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages