Hapana shaka viwango vya ubora katika kuwa na hofu ya Mungu, umakini na utendaji kazi uliotukuka wa Rais Dk. John Magufuli, ulipata kujulikana kwa watu wengi hata kabla ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ulijulikana tangu akiwa Naibu Waziri na Waziri kamili katika Wizara kadhaa ikiwemo Wizara ya Ujenzi na Wizara iliyokuwa ikishughulikia Uvuvi (sitaeleza kwa kirefu).
Kufuatia umahiri wake katika sifa nilizotaja hapo, watu wa kada mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania wamekuwa kila mmoja akijitahidi kumwelezea Rais Dk. Magufuli kwa namna mbalimbali ili kuonyesha anavyoridhishwa naye. Wapo wanaomwelezea kwa njia ya sanaa, wengine maandiko.
Miongoni mwa ambao wamekuwa wakiandika na kumsifu Rais Dk. Magufuli hadharani, ni Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba la Tegeta Dar es Salaam, ambaye anatambulika kwa jina la Baba wa Uzao kulingana na hadhi yake kiuongozi wa kanisa hilo.
Hapa ameandika andiko ambalo nimehabatika kulipata na kulisoma kwa makini na baada ya kulisoma nimehamasika kulichapisha katika Blog hii ya Taifa ya CCM, ili nawe mdau au pengine mwenyewe Rais Dk. Magufuli aweze kulisoma.
Lifuatalo ndilo andiko hilo la Baba wa Uzao kuhusu amuonavyo Rais Dk. Magufuli.👇
UFUNGUO
Ilikuwa saa 5:30 asubuhi lango la 22 Tamuzi, Vol. (7 Oktoba, 2020) niliposikia Sauti ikiniambia kuchukua Kalamu na kuandika yafuatayo kuhusu Rais Dkt Magufuli (Isaya 30:21):
1. Rais Dkt Magufuli ni Fahari ya Afrika
Wengi tulitamani kufundisha Ukarimu wa Waafrika, lakini hatukuwa na Chuo wala Mtaala wa kufundisha Somo hilo kwa wengine. Aidha, tulikuwa tunatamani kufundisha Maisha ya Kifamilia ya Mwafrika kwa wengine, lakini tulikuwa hatuna Chuo cha Familia ya Kiafrika wala Mtaala wake.
Pia, wengi walikuwa wanapenda kuwa na Uongozi unaofikia Jamii ambayo haiwezi kujitetea yenyewe lakini Chuo na Mtaala wake siyo rahisi kuvipata pamoja na kwamba kuna vyuo vingi vya Maendelo ya Jamii. Hata hivyo, ukifuatilia Hotuba na Misafara ya Rais Dkt Magufuli, unapata chuo na Mtaala wa hayo niliyoeleza hapo juu.
Sikuwahi kuona Rais anayekula kwenye Mgahawa wa Kawaida kijijini kama Rais Dkt Magufuli. Kubwa kuliko, sikuwahi kuona Rais anayekula na wananchi ambao wamesimama Barabarani kama Rais Dkt Magufuli. Kile kitendo cha kusimama kila mahali anapowakuta Wananchi wengi, kuwasalimia, kuwauliza shida zao na Wananchi kuwa huru kuongea naye kuzitatua shida zao papo kwa hapo, ni maisha ya Baba na Mwana wakiwa Nyumbani, yaani maisha ya kifamilia. Yeye anafanya kwa Wananchi wake wote. Zaidi sana, hiyo siyo elimu ya darasani, bali ni Isaya 57:15, yaani MUNGU BABA ndani yake.
2. Rais Dkt Magufuli ametuvika Vazi Waafrika wote
Kila anayesikia Bara la Afrika, aliona ambao wako uchi. Kuwa uchi ni kukosa ufahamu wa kubadilisha mazingira yaliyokuzunguka kuwa mazuri kwako na wengine. Hali kama hiyo ilitokea kwa Adamu wa Kwanza na Mkewe katika Mwanzo 3:7-8. Rais Dkt Magufuli ameifuta hiyo hali kwa Waafrika wote, kuonekana hawana ufahamu wa kubadilisha mazingira yaliyowazunguka.Ndiyo maana nasema amewavika Waafrika wote Vazi.
3. Rais Dkt Magufuli karejesha Heshima Afrika
Nimewahi kushuhudia kwa macho wasomi wakishushwa Cheo katika Mabara nje ya Afrika kwa kuwa ni Waafrika. Nina hakika sasa hivi hakuna atakayeshushwa Cheo kwa kuwa ni Mwafrika, baada ya Uumbaji wote kushuhudia umahili na ufahamu alionao Rais Dkt Magufuli. MUNGU BABA amwinue kupita kawaida (Kumbukumbu 28:8-14). Maana sote Afrika tunasikia kuheshimiwa kutokana na Mfumo wake.
4. Rais Dkt Magufuli amekuwa fimbo ya kuchapia waovu
Ile tabia ya kuishi Moyo, kusema Kweli, Kutekeleza yote anayoahidi; kutokuwa na Maslahi Binafsi, na Kumtanguliza Aliyetuumba sote, ni Fimbo Kubwa ya kuchapa waovu. Nina hakika, hakuna Kiongozi wa Ngazi yake ambaye aliwahi kumwinua MUNGU BABA hadharani kama Rais Dkt Magufuli. Kwa ajili ya hilo, alindwe Umilele wote (Isaya 43:4). Wale Waimbaji waliosema ni Baba lao, walikuwa wanamaanisha kuwa Rais Dkt Magufuli ni Kiongozi. Mataifa yote waandike jambo hili.
Kitendo cha Tanzania kuishinda korona wakati inasumbua Mataifa yote, siyo kawaida. Wasione aibu kuandika. Kama Ulaya; Amerika; Asia; Australia na New Zealand hawatandika, basi Bara la Afrika liandike kuhusu Rais Dkt Magufuli. Maana amekuwa fahari yetu sote.
Nahitimisha kwa kuongea na wale wenye maoni tofauti na haya ninayoandika; naomba hata wao wachambue na waseme katika haya kama si kweli tupu. Mimi katika Moyo ninaona kuwa tumepata Kiongozi ambaye ametutoa aibu Wafrika wote. HERI MLIOBARIKIWA NA MUNGU BABA.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇