Kamishna Msaidizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa, (TANAPA), Pascal Shelutete, amesema kuwa moto uliozuka na kuanza kuteketeza sehemu ya hifadhi za Mlima Kilimanjaro, huenda wakafanikiwa kuuzima hii leo baada ya hapo jana kushindikana na kuendelea kuwaka usiku kucha.
“Kama TANAPA tumefanya juhudi kubwa sana na asubuhi ya leo vikosi mbalimbali vimefika Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya zoezi hilo la kuuzima moto, kazi ya kuuzima moto huo inaendelea na tunatarajia kwa nguvu hiyo iliyopelekwa moto huo utaweza kudhibitiwa kuzima kwa siku ya leo” Shelutete
“Bado tunaendelea kufanya tathmini na baadaye tutatoa taarifa kamili juu ya chanzo na madhara ambayo yamejitokeza, kipaumbele kwanza tunashughulikia masuala ya uzimaji wa moto halafu mengine yatafuata baadaye” Shelutete
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇