Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akizungumza katika Maadhimisho ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Kanisa la Menonite mjini Songea mkoani Ruvuma.
Na Mwandishi Maalum Ruvuma
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewaomba viongozi wa Dini kuoimbea amani Tanzaniai kuelekea uchaguzi mkuu uliopagwa kufanyika Siku ya Jumatano, Oktoba 28,2020.
Mndeme ametoa ombi hilo katika Maadhimisho ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Kanisa la Menonite mjini Songea mkoani Ruvuma, ambapo pamoja na ombi hilo, alichangia tani tano za sariji yenye thamani ya sh. milioni 1.5 kwa ajili ya Ujenzi wa Kanisa hilo.
“Endeleeni kuiombea nchi yetu, tunasali hapa kwa sababu kuna amani wengine wanakimbia na masanduku na watoto kwa sababu hakuna amani katika nchi zao”, alisisitiza Mndeme.
Mndeme amewaomba wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na Watanzania kwa ujumla kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli pamoja na wasaidizi wake ili nchi ya Tanzania ipate maendeleo zaidi katika sekta mbalimbali.
Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la Moroviani Usharika wa Songea mjini Selemani Nzyemba akizungumza kwa niaba ya Mchungaji wa Kanisa la Menonite amemshukuru Mkuu wa Mkoa na timu yake kwa kwa msaada wa vifaa vya ujenzi.
Amesema msaada huo ni mkubwa kwa kanisa hilo ambao utasaidia kuendeleza ujenzi na kwamba pia amemshukuru kwa kuacha majukumu yake na kufika kushiriki katika ibada ya kuazimisha mwaka mmoja tangu kuanzisha kanisa hilo mjini Songea.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇