LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 11, 2020

ZANZIBAR WAUNGURUMISHA TAARAB MAALUM KUMPONGEZA DK. MWINYI, DK. SHEIN AHUDHURIA

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na Mgombea Urais wa Visiwa hivyo kwa tiketi ya CCM Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi wakati wa taarab maalum iliyoandaliwa na kuporomoshwa na Kikundi cha Culture Musicalna katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar jana usku kwa ajili ya kumpongeza mgombea huyo kwa kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika kinyang'anyiro cha Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi ujao.

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Visiwa hivyo kwa tiketi ya CCM Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi wakifurahia mirindimo ya taarab hiyo maalum ilivyokuwa ikiungurumishwa na Kikundi cha Culture Musical.

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Mke wa Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya CCM Mama Maryam Mwinyi (kushoto) wakifurahia mirindimo ya taarab hiyo,

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) na Mke wa Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya CCM Mama Maryam Mwinyi (kushoto) Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (kulia) wakimtunza muimbaji wa Kikundi cha Culture Musical Fatma Dawa Shehe, aliyekuwa akiimba wimbo wa “Tumtunze Dk. Shein” wakati wa taarab hiyo maalum

MSANII wa Kikundi cha Culture Musical Taarab Iddi Suwed akiimba wimbo wa “ Kama Kupenda Dhara” wakati wa hafla hiyo ya Taarab Maalum. 

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk. Hussein Mwinyi wakati wa taarab hiyo Maalum. Kushoto ni Mama Mwanamwema Shein na Mama Maryam Mwinyi

RAIS wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mke wa Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi Mama Maryam Mwinyi alipokuwa akiwasili kwenye taarab hiyo maalum. Kushoto ni Mama Mwanamwema Shein akisalimiana na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi. (Picha zote na Ikulu, Zanzibar) 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages