Na Scolastica Msewa, Mkuranga
Mgombea ubunge wa jimbo la mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega amewataka wananchi wilayani Mkuranga kuchagua maendeleo sio kufuata ushabiki wa vyama.
Ulega amebainisha hayo kwenye kampeni za jimbo katika kata ya Kisegese na Kimanzichana wilayani Mkuranga ambapo aliomba kura za wagombea wa Chama cha Mapinduzi.
Amesema kama wanataka maendeleo wachague wagombea wa Chama Cha Mapinduzi kuanzia Mgombea wa Urais Dr. John Pombe Magufuli, Mgombea Ubunge Abdallah Ulega na madiwani wa kata zote wa CCM.
Amesema wagombea wa Upinzani hawana mpango wa kuleta maendeleo bali ni ushabiki tu wa kupinga kila kinachofanywa na CCM.
Ulega amesema iwapo wananchi hao wa kata ya kimanzichana watachagua mafiga matatu ya CCM kazi ya kwanza kuifanya ni kufungua Zahanati ya kijiji cha kimanzichana ambayo kwa sasa ipo katika hatua ya kuweka umeme.
Amesema kwa sasa uongozi wa kata hiyo jukumu lao ni kutafuta nyumba nzuri ya kuishi mganga wa zahanati hiyo ambayo ataigharamia yeye badala ya kusubiri nyumba ya serikali ya mganga huyo kujengwa lengo likiwa ni wananchi wa kata hiyo wapate huduma za afya hapo hapo kimanzichana.
Kwa upande wa maliza tatizo la wingi wa watoto katika shule ya shule ya msingi kimanzichana Ulega amesema atatoa mifuko 300 ya sementi punde baada ya ushindi kwa mafiga matatu ya CCM ahadi ambazo vyama vya upinzani hawawezi kutimiza.
Aidha akizungumzia ujenzi wa shule ya msingi kimanzichana kusini Ulega amesema atatoa shilingi milioni 3 kwaajili ya kumalizia manunuzi ya kiwanja cha kujenga shule iwapo wananchi wa kata hiyo watachagua mafiga matatu ya CCM mara baada ya oktoba 28 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇