Simba SC leo imewakaribisha Biashara United ya Musoma katika uwanja wa Mkapa kukipiga katika muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu soka Tanzani bara 2020/21.
Biashara wakiwa ndio wageni wamekutana na kipigo cha magoli 4-0 kutoka kwa Simba SC ambaye ndio Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu.
Magoli ya Simba SC yalifungwa na Clatous Chama aliyefunga mawili dakika ya 9 na 26, Meddie Kagere dakika ya 52 na Mugalu aliyehitimisha kwa kupachika msumari wa mwisho dakika ya 85.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇