LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 7, 2020

MAJALIWA AMUUNGANISHA MGOMBEA WA UBUNGE CCM MOSHI MJINI NA MTIA NIA AMBAYE HAKUTEULIWA

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia Mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo na aliyekuwa mtia nia aliyeomba uteuzi wa CCM katika  jimbo hilo lakini hakuteuliwa, Ibrahim Shayo (kulia) wakiwa pamoja, baada ya kuwaunganisha katika Mkutano wa Kampeni aliohutubia katika Uwanja wa Majengo mjini Moshi jana. Ibrahim Shayo aliahidi hadharani kuwa atamuunga mkono mwenzake Tarimo.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Moshi Mjini, Priscus Tarimo (kushoto) akikumbatiana  na mtia nia wa uteuzi wa CCM katika kugombea nafasi hiyo ambaye hakuteuliwa , Ibrahim Shayo wakati Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowakutanisha kwenye jukwaa kuu na kuwasihi wavunje ukimya, Wakati wa Mkutano wa Kapeni uliofanyika jana katika Uwanja wa Majengo mjini Moshi. Ibrahim alitamka hadharani kuwa atamuunga mkono mgombea wa CCM Tarimo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages