LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 7, 2020

DK. OSCAR KIKOYO: NICHAGUENI ILI NISIMAMIE ILANI YA CCM NA VIPAUMBELE VYANGU

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika  Jimbo la Muleba Kusini Dk. Osca Kikoyo akisalimia wananchi wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kampeini za CCM uliofanyika jana mjini Muleba.

Na Alodia Babara, Muleba

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Muleba Kusini Dk. Oscar Kikoyo ameomba wananchi kumchagua ili asimamie  vipaumbele anavyoviahidi katika kipindi hiki cha kuomba kura moja wapo ikiwa ni kusogeza huduma ya maji karibu na kumtua mama ndo kichwani.


Akihutubia wananchi waliohudhuria kwa wingi katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Red Cross mjini Muleba Dk Kikoyo alisema Sera ya maji inayotolewa na Serikali ya awamu ya tano itasaidia huduma hiyo kusambazwa jimbo zima la Muleba kwa kujenga visima vidogo vidogo ambavyo vitasaidia kumtua mwanamke ndoo kichwani.


Ameeleza kuwa, ujenzi wa visima hivyo itakuwa ni mwendelezo wa ujenzi wa miradi ya maji ambayo imetekelezwa kwa kipindi Cha miaka mitano iliyopita ya kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi na kuacha kutembea mwendo mrefu kufuatia maji.


Ametaja maeneo mengine kuwa ni ujenzi wa shule za sekondari kidato cha tano na sita katika maeneo tofauti ya jimbo hilo pamoja na kuweka nguvu katika ujenzi wa vyumba vya madarasa. 


Kipaumbele kingine ni pamona na Afya kwa kujenga na kuboresha zahanati na vituo vya afya na miundombinu ya barabara na kuwaahidi wananchi uwakilishi shirikishi na kuimarisha mipango ya kuongeza makusanyo kutoka vyanzo mbalimbali ili yatumike kuchochea maendeleo ya wananchi.


Mbunge wa zamani wa Jimbo hilo ambaye hakugombea tena nafasi hiyo Profesa Anna Tibaijuka alisema kwa kumpata Dr Oscar Kikoyo anaamini jimbo analiacha katika mikono salama na kuwa katika uongozi wake ametoa mchango mkubwa katika maeneo tofauti.


Katika mkutano huo aliyekuwa Mwenezi wa Wilaya kupitia Chadema Kassim Mustafa alirejea CCM akisema kuwa anaunga mkono kazi iliyofanyika kwa miaka mitano iliyopita na kuwa yuko tayari kushirikiana na wagombea waliopitishwa na CCM kutafuta kura na kushirikiana nao kutafuta maendeleo ya jimbo hilo.


Aidha mkutano ulihudhuriwa na mgombea Ubunge wa Muleba Kaskazini Charles Mwijage aliyesema kasi ya maendeleo katika Wilaya hiyo itaongezeka zaidi na kuwaomba wananchi kuwachagua ili wasimamie utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.


Dk. Kikoyo ni Mwanasheria na wakili wa kujitegemea ambapo pia ni Mhadhiri wa muda katika vyuo vikuu tofauti nchini  na  ametumikia nyadhifa tofauti za uongozi Serikalini.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages