LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 18, 2020

BAADA YA TURKY KUFARIKI DUNIA MWANAE ABEBA MIKOBA KUGOMBEA JIMBO LA MPENDAE KWA TIKETI YA CCM


Tawfiq Salim Turky

Baada ya Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Mpendae Zanzibar Salim Hassan Abdullah Turky (Mr White) kufariki dunia hivi majuzi, kimemteua mwanae Tawfiq kuwa mgombea wake katika Jimbo hilo.

Turky ambaye ambaye alikuwa Mbunge wa jimbo hilo katika kipindi kilichopita cha 2015-2020, amefariki dunia katika Hospitali ya Global alikopelekwa baada ya kuugua hafla.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mgombea ubunge wa chama chochote cha Siasa anapofariki ndani ya siku 30 za mwanzoni mwa kampeni chama husika hupewa nafasi ya kuteua mgombea mwingine na anapofariki nje ya siku hizo uchaguzi huahirishwa katika jimbo husika.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages