LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 25, 2020

RIDHIWANI KIKWETE ATEULIWA NA NEC KUWA MGOMBEA UBUNGE CHALINZE KUPITIA CCM + VIDEO


Mgombea ubunge mteule wa Jimbo la Chalinze, mkoani Pwani, Ridhiwan Kikwete (kulia) akirejesha fomu kwa Msimamizi wa Uchaguzi 2020, Mkurugenzi wa Chalinze, Ramadhan Possi na baadaye kuteuliwa kugombea jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu ambao kampeni zake zinaanza Agosti 26 na kumalizika Oktoba 27 mwaka huu. 
Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM waliojitokeza kumsindikiza.
 NA ANDREW CHALE, CHALINZE.

KADA wa Chama Cha Mapinduzi CCM na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete leo 25 Agosti, amerejesha fomu ya kugombea Ubunge jimbo hilo kwa mara nyingine tena.

Ridhiwani amerejesha fomu hizo na kupokelewa kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Chalinze, Ramadhan Posi.

Ridhiwani amesema wamejiandaa kufanya kampeni za staa ambazo zitakuwa za  kunadi sera na kuendeleza yale aliyoanzisha awali."CCM imejipanga kuendeleza kampeni za kistaarabu. Sisi hapa Chalinze Kazi inaendelea."Alisema Ridhiwani.

Miongoni mwa mambo atakayoendeleza ni pamoja na miundombinu, elimu, afya na maji.Pia amesema kumalizia kiporo cha Kituo cha Afya Kibindu pamoja na  kumalizia Hospitali ya Wilaya ya Chalinze katika awamu zake nne zilizobaki.

"Tunataka suala la maji liwe la mfano kwani awali hapakuwa na huduma za maji Chalinze. kwa sasa tumepiga hatua maji yanapatikana katika karibu vijiji vingi. Lakini pia kuweka utaratibu wa maji yale yaweze kuleta vipato kwa Wananchi." Alisema Ridhiwani.

Aidha, amesema msemo wa "Kazi zinaendelea"  ni kwa sasa ni hatua ya kuubadilisha mji wa Chalinze na kuwa wa mfano  ikiwemo miundombinu ya kisasa pamoja na ujenzi wa stendi ya mabasi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages