Ofisa Mauzo Ezekiel Kwaka (kulia), akitoa maelezo kuhusu ubora wa Mkaa Mweupe wakati wa Maonesho ya Wakulima ya Nanenane Kanda ya Kati kwenye viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma yaliyomalizika hivi karibuni. Mkaa huo ambao ni rafiki wa mazingira ulikuwa unauzwa kwenye mifuko sh.3000 (vipande 30) na 5000 (vipande (50) na 20000 (vipande vikubwa 25).
Vipande vya Mkaa Mweupe vidogo na vikubwa ambapo vidogo hutumika kwa majiko madogo na vikubwa kwa majiko makubwa.
Aristotle Nikitas Meneja Masoko wa Kampuni ya Premium Active Tanzania Limited, inayotengeneza Mkaa Mweupe, akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Singida, Dk. Rehema Nchimbi baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi wa pili kundi la Wajasiriamali na Wawekezaji wadogo wakati wa kilele cha Maonesho ya Wakulima ya Nanenane Kanda ya Kati kwenye viwanja vya Nzuguni, Dodoma.
Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Ofisa Mauzo, Ezekiel Kwaka akielezea kuhusu matumizi ya vipande vidogo vya mkaa ambapo alisema kati ya vipande vitatu au vinne kupika vyakula kwa takribani masaa manne bila kuzimika. Mfuko mmoja wenye vipande vidogo 30 huuzwa sh.3000.
Mkaa Mweupe hutengenezwa kwa kutumia majani maalumu
Jiko kubwa linalotumia vipande vikubwa vya Mkaa Mweupe ambalo lilikuwa linaoneshwa jinsi mkaa huo unavyoivisha kande. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Aug 13, 2020
MKAA MWEUPE WAPOKEWA NA WANANCHI KWA MOYO MWEUPE
Tags
featured#
Mazingira#
Share This

About Richard Mwaikenda
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇