Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli leo tarehe 18 Julai, 2020 amemteua Dkt. MwinyiTalib Haji
kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Haji alikuwa Mkurugenzi wa
Chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar
na anachukua nafasi ya Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi.
UteuziwaDkt. Haji unaanza leo tarehe 18 Julai,
2020 na anatakiwa kuwepo Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Julai, 2020 saa
4:00 asubuhi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇