Katibu Mwenezi na Itikadi wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu (kulia) akitoa
taarifa jana kuhusu idadi ya wagombea ubunge wa chama hicho, Mkoa wa
Singida waliorudisha fomu. Kusho ni Katibu wa UVCCM wa mkoa huo, George
Silindu.
Afisa kutoka TAKUKURU Mkoani hapa, Samson Julius akitoa mada kwa wagombea hao.
Wagombea Ubunge wa chama hicho, Mkoa wa Singida wakiwa katika semina ya kutojihusisha na vitendo vya rushwa iliyotolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani hapa.
Wagombea Ubunge wa chama hicho, Mkoa wa Singida wakiwa katika semina hiyo.
Wagombea Ubunge wa chama hicho, Mkoa wa Singida wakiwa katika semina hiyo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
WAGOMBEA nafasi
ya Ubunge wa Majimbo na wa viti Maalumu 283 wamekwisha rudisha fomu za
kuomba ridhaa ya kupitishwa kugombea nafasi hizo huku Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani hapa ikitoa onyo kwa wagombea kutojihusisha na vitendo vya rushwa.
Katibu Mwenezi na Itikadi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu akitoa taarifa hiyo jana
kwa waandishi wa habari alisema mkoa huo una jumla ya majimbo nane
ambapo katika nafasi ya ubunge wa majimbo pekee ni wagombea 233, huku
viti maalumu wakiwa 51.
Katika Jimbo la Singida mjini
waliojitokeza kugombea nafasi ya ubunge ni 30 kati yao wanawake 2,
Singida kaskazini ni 34 kati yao wanawake 3, Singida mashariki ni 10 na
Jimbo la Singida magharibi ni 14.
Jimbo la Iramba magharibi waliojitokeza
ni wagombea 30 kati yao wanawake 3, Iramba mashariki ni 51 kati yao
wanawake 2, Manyoni mashariki ni 35 kati yao wanawake 4 na Manyoni
magharibi ni wagombea 24.
Upande wa ubunge viti maalumu jumuiya za CCM,Uwt 44,Vijana 6 na upande wa jumuiya ya wazazi amejitokeza mgombea mmoja pekee.
Aidha kaburu alisema taratibu zote za
uchaguzi zimeshakamilika ambapo uchaguzi kwa upande wa majimbo
utafanyika July 20, UWT July 23, UVCCM July 30,na jumuiya ya wazazi ni
July 31 mwaka huu.
Hata hivyo wagombea wote 30 wa ubunge
wa jimbo la Singida mjini baada ya kukamilika zoezi la kurejesha fomu
walipata fursa ya kukutana na Maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa (TAKUKURU) mkoani hapa na kukumbushwa kufuata taratibu za
uchaguzi.
Afisa kutoka TAKUKURU Mkoani hapa,
Samson Julius akitoa mada kwa wagombea hao baada ya kurudisha fomu
alitoa onyo kutojihusisha na vitendo vya rushwa na kujikuta wanaingia
kwenye mikono ya TAKUKURU.
"Zingatieni maadili kwa kufuata taratibu vinginevyo mtajikuta mpo mikononi mwa ( TAKUKURU) alisema Julius.
Alisema TAKUKURU haitaogopa kumchukulia hatua za kisheria mgombea yeyote atakaye kiuka maadili na kushindwa kufuata taratibu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇